SINGIDA, TANZANIA
Mtu mmoja amekufa baada ya kupigwa kufuatia vurugu kubwa zilizotokea kwenye mkutano wa Chadema eneo la Iguguno mkoani, Singida. Imeripoti TBC 1 usiku huu.
Mwandishi wa kituo hicho, aliyeko Singida, Leonard Manga amesema mrtu aliyeuawa alikimbizwa na wafuasi wanaosadikiwa kuwa wa Chadema ambaoa walimfuata hadi katika nyumba alimokimbilia ambako walimpiga hadi kumuua.
Amesema chanzo ni furugu zilizotokea kwenye mkutano wa Chadema uliofanyika eneo la Iguguno, ambazo kwa mujibu wa mtangazaji huyo zilisababishwa na Chadema kutoa maneno ya kumkashifu mbunge Mwigulu Nchemba, jambo ambalo anadai lilisababisha watu waliopinga matusi hayo walivurumisha mawe kwenye mkutano huo na kusababisha tafrani.
"Nadhani wale waliorusha mawe watakuwa ni wana-CCM ambao inaonekana walichukizwa sana na maneno yaa kashfa yaliyokuwa yakitolewa na Chadema kwenye mkutano huo dhidi ya Nchemba", alisema Mtangazaji wa TBC 1
Aliongeza; " wakati watu wakikimbia huku na huko naaba ya vurugu kuwashinda polisi , mtu mmoja alikimbilia kwenye nyumba moja lakini Chadema waliokuwa wanamkimbiza walimfuata na kumpiga hadi kumuua papo hapo".
Amesema, kufuatia tukio hilo watu kadhaa wamekamatwa lakini haijathibitishwa kama ndiyo wanaohusika hasa na vurugu hizo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269