Wataalam kutoka Tanzania ambao kutokana ukumbi uliotengwa kufanyika mkutano huo kuwa mdogo kuliko idadi ya wahudhuriaji walilazimika kukaa ukumbi mwingine ambao umeandaliwa mahususi kwaajili ya kufuatili kwa njia ya Video kile kilichokuwa kikijili katika ukumbi mwingine. kutoka kushoto ni Brigedia Jenerali Venance Mabeyo ( JWTZ), Kamishna Esaka Mugasa,(Polisi) , Meja Wilbert Ibuge (mwambata Jeshi Ubalozini), Wakili John Kinuno kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Bw. Theobald Kazora, kutoka Idara ya Mambo ya Nje ( Ofisi ya Rais)Brigedia Generali Dkt. Charles Muzanila kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) akifuatilia kwa makini majadiliano yanayoendelea kuhusu kuanzishwa kwa Mkataba wa Kisheria wa Biashara ya Silaha Duniani (ATT) mkutano huu muhimu unafanyika hapa Umoja wa Mataifa. Ukiwa umeingia wiki yake ya pili tayari mataifa mengi ambayo yamekwisha kuchangia majadiliano hayo, yameelezea misimamo yao ikiwamo ya kutouridhia Mkataba huo endapo utakuwa na mwelekeo wa kubinya uhuru wa nchi kulinda watu wake na mipaka yake, au kama utakuwa unaingilia uhuru wa nchi kujiamulia mambo yake. Baadhi ya mataifa yamekuwa yakisisitiza kwamba mkataba huo lazima pia uzibane nchi zinazozalisha silaha hizo badala ya kulenga tu nchi zinazonunua. vilevile mataifa mengi yamesisitiza uwazi na ukweli katika mchakato mzima wa majadiliano hayo. mkutano huu ni wamwezi mmoja HABARI KAMILI INGIA TANZANIA VISION BLOG... BOFYA HAPA
Your Ad Spot
Jul 10, 2012
Home
Unlabelled
MKUTANO WAJADILI KUANZISHWA MKATABA WA KISHERIA WA BIASHARA YA SILAHA DUNIANI (ATT) WAFANYIKA MJINI NEW YORK
MKUTANO WAJADILI KUANZISHWA MKATABA WA KISHERIA WA BIASHARA YA SILAHA DUNIANI (ATT) WAFANYIKA MJINI NEW YORK
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269