Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Jan Eliasson akisaini kitabu cha Maombolezo ambacho kimefunguliwa katika Ubalozi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa. Katika Salamu zake, Naibu Katibu Mkuu ameelezea kuguswa kwake na tukio la ajali ya kuzama kwa meli na hasara iliyotokana na ajari hiyo ikihusisha pia kupotea kwa maisha ya watu. Mhe. Jan Eliasson ni miongoni mwa wanadiplomasia ambao wamekuwa wakifika kutoa salamu zao za pole na kuungana na watanzania katika kipindi hiki cha majonzi.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Jan Eliasson akizungumza na Kaimu Balozi, Dkt. Justin Seruhere mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo ambapo alielezea namna gani anavyoifahamu Tanzani na mapenzi yake makubwa kwa nchi hiyo na kwamba ni kama miaka miwili tu iliyopita alikuwa Kisiwani Zanzibar. Katika salamu zake za pole Mhe. Elliasson amesema sala na dua zake anazielekeza kwa wahanga wa tukio hilo, Serikali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na kwamba Umoja wa Mataifa uko pamoja na watanzania katika kipindi hiki kigumu.
Your Ad Spot
Jul 21, 2012
Home
Unlabelled
UN YAOMBOLEZA MAAFA YA KUZAMA MELI ZANZIBAR
UN YAOMBOLEZA MAAFA YA KUZAMA MELI ZANZIBAR
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269