JIBABA lenye umri wa miaka 40, limehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na kutandikwa viboko 12, baada ya kupatikana na hatia ya kubaka mwanafunzi mwenye umri wa miaka 12.
Jibaba hilo, linaloitwa Feja, mkulima wa kijiji cha Sanzake, wilayani Bunda mkoani Mara, amehukumiwa adhabu hizo leo, na mahakama ya wilaya ya Bunda.
Mapema, mwendesha wa polisi Masoud Mohamed, alisema kwamba mei 22 mwaka huu, mida ya saa 6 mchana, katika kijiji cha Rakana wilayani Bunda, mshitakiwa huyo alimbaka mtoto huyo wakati mtoto huyo baada ya kumfuatilia wakati akienda kuchota maji kisimani na ndipo alimvutia vichakani ambako alimvua ngou na kumbaka.
Aliendelea kusema kuwa baada ya mtoto huyo kubakwa alipiga kelele za kuomba msaada na wananchi wakafanikiwa kufika katika eneo la tukio, na ndipo wakamkamata mtuhumiwa huyo ana kumfikisha polisi.
Akitoa hukumu hiyo hakimu wa mahakama ya wilaya ya Bunda, Safina Simfukwe, alisema kuwa ameridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashitaka pasipo kuwa na shaka yeyote.
Hakimu Simfukwe alisema kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashitaka, amelidhika nao pasipo kuacha shaka yoyote, hivyo anamtia hatiani mtuhumiwa huyo, kutumia kifungo cha miaka 30 jela na kuchapwa viboko 12, ili liwe fundisho kwake na kwa watu wengine wenye nia ya kufanya vitendo kama hivyo.
Kabla ya kutolewa hukumu mshitakiwa huyo alipewa nafasi ya kujitetea ambapo aliiomba mahakama hiyo impunguzie adhabu kwa vile anayo majukumu mengi yanayomkabili, hata hivyo hakimu Simfukwe aliutupilia mbali utetezi huo, baada ya upande wa mashitaka kuiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa huyo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269