MWENYEKITI UVCCM TAIFA |
ARUSHA, Tanzania
MWENYEKITI wa Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi
Taifa (UVCCM), Sadifa Juma Hamisi, amepinga vikali kuwepo kwa mfumo wa serikali
tatu kama inavyopendekezwa katika rasimu ya katiba.
Sadifa ameyasema hayo wakati akizungumza na wanachama wasomi wa UVCCM kutoka katika vyuo vikuu mkoani kilimanjaro katika hafla ya kuwaaga wasomi hao na ambapo pia ametunuku vyeti vya uanachama kwa wanafunzi 312 pamoja na kuwakabidhi kadi za uanachama wanachama wapya.
Mwenyekiti huyo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Donge (CCM) zanzibar, amesema uwepo mfumo wa serikali tatu ni mzigo mkubwa kwani kutokana na uduni wa uchumi wan chi yetu itakuwa vigumu kuendesha serikali tatu kwa maana ya serikali ya Zanzibar, serikali ya Tanzania bara na ule wa muungano. HABARI NA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269