Uswizi mmh! Messi, Angel Di Maria na Ezequiel Lavezzi wakishangilia ushindi kwenye chumba cha kubadilishia nguo.
LIONEL
Messi amekiri kuwa Argentina walibanwa sana kabla ya Angel Di Maria
kufunga bao pekee dhidi ya Uswisi katika dakika za nyongeza lililowapa
tiketi ya kwenda robo fainali ya kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
"Wote
tulihangaika, tulihangaika na kuhangaika,' alisema Messi. "Tulianza
kuwaza kama haitatokea. Lakini mwisho bahati ilituangukia na tunatakiwa
kutumia faida hiyo kusonga mbele".
"Kama
ilivyokuwa kwa wote, niliumia sana kwasababu sikufunga. Tulijua kama
tungefanya kosa moja tungerudi nyumbani. Hatukutaka kusubiria penati.
Tulitaka kumaliza dakika za kawaida".
Mashabiki bab kubwa!: Mpenzi wa Messi, Antonella Roccuzzo na mtoto wao wa kiume Thiago wakitazama ushindi wa Argentina.
Mpe busu hili baba yako: Messi mdogo akipata busu kutoka kwa mama yake baada ya baba yake kutengeneza bao la ushind.
==========
MAREKANI YAPIGWA 2-1 NA UBELGIJI, LAKINI KIPA WAO ATIA FORA.
Kijana wa kazi: Howard aliokoa michomo mingi zaidi ukilinganisha na kipa mwenzake wa Ubelgiji, Thibaut Courtois
Howard akijitanua na kuokoa mpira uliopigwa na nahodha wa Ubelgiji Vincent Kompany
Kwa
kuokoa michomo 15, kipa huyo wa Everton ameandika rekodi mpya ya kombe
la dunia tangu takwimu kama hizo zipatikane mwaka 1966 ambapo kipa wa
Peru, Ramon Quiroga aliokoa michomo 13 mwaka 1978 dhidi ya Uholanzi.
Kiwango
cha jana cha Howard ndio bora zaidi kuwahi kutokea katika timu ya
Marekani tangu Sylvester Stallone afanye hivyo mwaka 1981.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269