Breaking News

Your Ad Spot

Jul 1, 2014

NIGERIA YARUDISHA MACHUNGU AFRIKA, YATANDIKWA 2-0 NA UFARANSA, YOBO AJIFUNGA GOLI LA HASARA!

article-2675461-1F479A7300000578-129_634x431
Paul Pogba akirudi juu na kupiga kichwa  akiifungia Ufaransa bao la kwanza dhidi ya Nigeria.
NIGERIA maarufu kama Super Eagles imetupwa nje ya kombe la dunia baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Ufaransa usiku huu katika mchezo wa hatua ya 16.
Paul Pogba aliifungia Ufaransa bao la kuongoza katika dakika ya 78, huku beki wa Nigeria,  Joseph Yobo akijifunga bao katika dakika za lala salama mjini Brasilia.
article-2675461-1F479B4B00000578-353_634x394
Paul Pogba akinyosha vidole juu baada ya kuifungia Ufaransa.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

COUTINHO AANGUKA MKATABA WA MIAKA MIWILI YANGA SC

Andrey Coutinho akisaini mkataba wa kuitumikia Yanga kwa kipindi cha miaka miwili mbele ya Katibu Mkuu Beno Njovu leo makao makuu ya klabu

Kiungo mshamabuliaji Andrey Marcel Ferreira Coutinho raia wa Brazil leo amesaini mkataba wa miwili kuitumikia timu ya Young Africans kwa ajili ya michuano mbalimbali ikiwemo ya Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Katibu mkuu wa Young Africans  Bw Beno Njovu amesema usajliwa mchezaji Coutinho ni sehem ya muendelezo wa maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu na kama ilivyokawaida wao mambo yao ni kimyakimya.

Coutinho ambaye alizaliwa tarehe 12 Januari 1990 amekulia kwenye mji wa Berem ambapo alianza kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Paysandu Sports Club kabla ya kwenda nchini Asia katika nchi ya Myanmar katika klabu ya Rukhapura United

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages