Mlinzi wa timu ya Liverpool Kolo Toure amethibitisha kuwa amestaafu kucheza soka la kimataifa wakati akiwa na timu yake ya Ivory Coast iliyotwaa kombe la Mataifa ya Afrika AFCON.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 33 aliweka wazi kuwa mchezo wake wa mwisho
kuonekana uwanjani ulikuwa dhidi ya timu ya Equatorial Guinea.
Kolo
anasema anaipenda nchi yake na hasa anachokipenda zaidi maishani mwake
ni Kandanda,lakini amesisitiza kuwa huu ni wakati wake wa kusitisha
kuendelea kucheza.
“Najisikia
vibaya sana kuwafahamisha kuwa ni wakati wangu kuwaaga,Lengo langu
lilikuwa kushinda katika michuano ya kombe la mataifa ya Africa, na
nakubali ulikuwa ni uamuzi mgumu kutangaza“:- Kolo Toure.
Toure
amekuwa kiungo muhimu sana katika kuutengeneza ushindi wa timu na taifa
lake katika kipindi cha miaka ya 2006, 2010 and 2014 akiwa na kikosi
cha timu yake ya taifa katika michuano ya kombe la dunia.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269