Balozi
wa Japan nchini, Mh. Masaki Okada (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa
Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Hussein Kidanto wakitiliana saini
mkataba wa fedha za ruzuku shilingi milioni 70/ zilizotolewa na serikali
ya Japan kwa ajili ya kununua magari mawili ya wagonjwa (Ambulance).
Tukio hilo lilishuhudiwa na viongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili
pamoja na Mkurugenzi wa Hospitali hiyo aliyemaliza muda wake Dkt. Marina
Njelekela.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
…………………………………………………………………..
Waziri
wa Ujenzi Dk. John Magufuli ameishukuru Japan kupitia Balozi wake
alioko nchini kwa kusaidia miradi inayochangia maendeleo ya moja kwa
moja hususani afya, elimu na maji.
Dk.
Magufuli alisema hayo jana katika makazi ya Balozi wa Japan Nchini,
Masaki Okada yaliyopo Masaki Jijini Dar es Salaam wakati wa kutiliana na
saini za mkataba wa fedha za ruzuku zitakazoenda kusaidia maendeleo kwa
jamii ikiwemo Jimbo la Chato na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Katika
hafla hiyo, Dk. Magufuli aliambatana na viongozi mbalimbali akiwemo
Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Wilaya ya Chato, pamoja na Wakurugenzi
wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akiwemo Mkurugenzi wa zamani wa
hospitali hiyo Dk. Marina Njelekela pamoja na wa sasa Dk. Hussein
Kidanto.
Dk.
Magufuli alishuhudia utiaji wa saini wa mikataba hiyo ambapo Balozi
Okada alitoa kiasi cha sh milioni 70, kwa ajili ya ununuzi wa magari ya
kisasa ya kubebea wagonjwa (Ambulance) kwa Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili ambayo mpaka sasa inadaiwa wana Ambulance moja pekee.
Mbali
na kiasi hicho cha fedha, Pia Dk. Magufuli alishuhudia utiaji wa saini
huo ambapo Balozi huyo alitoa sh milioni 165, kwa ajili ya kujenga
kiwanda cha kukamulia mafuta ya Alizeti yenye viwango vya Kimataifa.
Dk.
Magufuli alishukuru kwa niaba ya Serikali na pia akiwa kama Mbunge wa
Chato, alisema Japan imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia juhudi za
maendeleo kwa wananchi mbalimbali wa mijini na vijijini.
Hata
hiyvo Dk. Magufuli alishtushwa na hali ya Hospitali hiyo ya Taifa kuwa
na Ambulance moja pekee wakati wao Halmashahuri ya Chato hadi sasa
wameweza kuwa na Ambulance tatu.
Balozi
wa Japan nchini, Mh. Masaki Okada (kulia) na Mkurugenzi wa Halmashauri
ya wilaya ya Chato mkoani Geita, Ndugu Clement Berege wakitiliana saini
mkataba wa fedha za ruzuku shilingi milioni 165 kwa ajili ya kujengea
kiwanda cha kukamulia mafuta ya Alizeti wilayani Chato mkoani Geita.
“Nimeshtushwa
sana na hili la kusikia kuwa mna Ambulance moja pekee. Yaani hata Chato
pale tuna Ambulance tatu. Naomba Mkurugenzi mpya, uendelee kuomba kwa
mabalozi wengine ili tuweze kupata Ambulance nyingi zaidi pia wanahabari
mtusaidie kwa hili.” Alisema Dk. Magufuli.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Chato, alipogeza Japan, kwa msaada wao kwani
utaenda kusaidia Halmashauri ya Chato kama ulivyokusudiwa.
“Wakazi
wa Chato ni wakulima, wafugaji na wavuvi, hivyo kwa msaada huu pia
utakuwa chachu ya maendeleo hasa kwa kilimo cha Alizeti.” Alisema
Mkurugenzi huyo.
Mbunge
wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli akitoa
shukrani kwa serikali ya Japan inayowakilishwa na Balozi Masaki Okada
baada ya kushuhudia utiaji saini wa mikataba ya fedha za ruzuku shilingi
milioni 235 sawa na dola za Kimarekani 136,015 zilizotolewa na serikali
ya Japan.
Japan
imekuwa ikisaidia mara kwa mara wilaya ya Chato, ambapo mwaka 2013,
Japan walitembelea huko na kujionea shida mbalimbali kwa wakulima wa
Alizeti hivyo wameona kusaidia msaada huo.
Mbali
na kusaidia mashine hiyo ya Alizeti Japan pia imekuwa ikisaidia
maendeleo mbalimbali ikiwemo shule za msingi, Sekondari na huduma za
afya kwa Hospitali iikwemo wodi ya akina mama.
Mkuu
wa wilaya ya Chato, Bw. Rodrick Mpogolo akizungumza kwenye hafla hiyo
ambapo pia alimshukuru Balozi Mh. Masaki Okada kwa kutengeneza ajira
wilayani kwake kupitia msaada huo.
Pichani
juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa na waandishi wa habari
waliohudhuria hafla hiyo fupi iliyofanyika nyumbani kwa Balozi Mh.
Masaki Okada jana jijini Dar.
Mbunge
wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli akiteta
jambo na Balozi wa Japan nchini, Mh. Masaki Okada mara baada ya hafla
fupi ya utiaji saini wa mikataba ya fedha za ruzuku kwa ajili ya
kuendeleza miradi inayochangia maendeleo ya moja kwa moja nchini.
Waziri
wa Japan nchini, Mh. Masaki Okada akiwa kwenye picha ya pamoja na
uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mara baada ya kuhitimisha
zoezi la utiaji saini wa mkataba wa fedha za ruzuku kwa ajili ya kununua
magari mawili ya wagonjwa (Ambulance) zilizotolewa na serikali ya
Japan.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269