Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na viongozi
na wajumbe wa Mfuko wa Changamoto za Millenia Tanzania (MCA-T) wakiongozwa na mwenyekiti
wake ambae pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Dr. Servaciaus Likwelile (kulia) ofisini kwake leo tarehe 12 Februari 2015. Katika
salam zake ameishukuru Serikali na mfuko huo kwa kazi nzuri inayofanyika Mkoani Rukwa na taifa kwa ujumla hususani katika ujenzi wa miundombinu ya barabara za lami, Pamoja na hayo
ameiomba Serikali na wafadhili wa MCC kusaidia pia katika ujenzi wa barabara
muhim za Wampembe iliyopo Wilaya ya Nkasi, barabara ya bondeni kwa ajili ya
kuunganisha ukanda wa bonde la Ziwa Rukwa unaoongoza kwa uzalishaji wa mpunga
na Mikoa ya Katavi na Mbeya, barabara ya Kasesha kwa ajili ya kuunganisha Mkoa
wa Rukwa na Zambia na barabara ya kuelekea Kalambo Falls yalipo maporomoko ya
Mto Kalambo ambayo ni ya pili kwa urefu barani Afrika.

Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (kulia) akiendesha kikao ofisini
kwake mapema leo tarehe 12 Februari 2015 kati yake na viongozi na wajumbe wa Mfuko wa Changamoto za Millenia Tanzania (MCA-T) .
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akitoa zawadi ya kanga kwa Katibu Mkuu Wizara ya fedha na uchumi Dr. Servaciaus Likwelile pamoja na viongozi wengine na wajumbe wa Mfuko wa Changamoto za Millenia Tanzania (MCA-T), Kanga hiyo ni ishara ya mafanikio ya miaka 40 ya Mkoa wa Rukwa 1974-2014.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa (kulia) alipata fursa ya kuwaalika viongozi na wajumbe wa Mfuko
wa Changamoto za Millenia Tanzania (MCA-T) kwa ajili ya chakula cha
usiku walipowasili Mkoani Rukwa tarehe 11 Februari 2015. Anaechukua
chakula ni Mwenyekiti wa mfuko huo ambae pia ni Katibu Mkuu Wizara ya
fedha na Uchumi Dr. Servaciaus Likwelile.
Picha ya pamoja.
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269