Kutoka kushoto ni Ofisa habari wa
Red Arrows Lt Melody Siisii, Mwenyekiti wa Red Arrows Col Nolasco
Chilando, Katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa na Ofisa Ubalozi wa
Zambia nchini Tanzania Alex Chila, wakiwa ofisi za TFF – PPF Tower leo.
…………………………………………………………………………………………………..
Klabu ya Red Arrow FC inayoshiriki
Ligi Kuu nchini Zambia inatarajiwa kuwasili jijini Dar es
salaam-Tanzania jumatatu ya wiki ijayo kwa ajili ya kuweka kambi ya
mafunzo ya wiki moja kujindaa na msimu mpya wa Ligi Kuu nchini humo
2015.
Uongozi wa klabu hiyo chini ya
mwenyekiti wake Col Nolacso K Chilando ulifika leo makao makuu ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania – TFF sambamba na Afisa
habari wa klabu Lt Col Melody Siisii, Bw Alex Chila ofisa ubalozi wa
Zambia nchini Tanzania kujitambulisha uwepo wao nchini.
Wakiongea na katibu mkuu wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania – TFF Selestine Mwesigwa,
uongozi wa timu hiyo umesema maandalizi ya kambi yameshakamilika na
kikubwa walikua wanaliomba Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini kutambua
uwepo wao na kuwasaidia kupata viwanja vya kufanyia mazoezi.
Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu nchini -TFF Bw.Mwesigwa alisema wameyapokea maombi hayo
ya Red Arrow FC na kuwakaribisha nchini kwa ajili ya kambi yao na
kusema ujio wao utafungua milango kwa vilabu vingine pia kuja kuweka
kambi nchini.
Timu ya Red Arrow FC inayomilikiwa
na jeshi la Anga nchini Zambia ikiwa nchini kwa mafunzo, inatarajia
kucheza mchezo mmoja wa kirafiki na imeliomba Shirikisho la Mpira wa
Miguu nchini kuwatafutia timu moja ya kucheza nayo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269