Mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha demokrasia na maendeleo chadema CHIKU ABWAO akikagua jengo lilokumbwa na ajali ya moto
Mbunge CHIKU ABWAO akiwa katika eneo la nje ya jengo liloungua
Mbunge
wa viti maalumu kupitia chama cha demokrasia na maendeleo chadema CHIKU
ABWAO alisikitiswa na uongozi wa shule ya sekondari ya idodi kushindwa
kumpokea kama mbunge na mama aliyeguswa na ajali ya moto katika shule
kwa kuwa alikuwa ameshatoa taarifa kabla hajaenda katika shule hiyo.
Kitendo
hicho kiliwafanya baadhi ya wanahabari wa manispaa ya iringa waliokuwa
wameongozana na mbunge huyo walikasilishwa kitendo kilichofanywa na
uongozi wa shule ya sekondari ya idodi na walianza kuhoji je? angekuwa
mkuu wa mkoa,mkuu wa wilaya na waziri au mbunge wa jimbo hilo
wangemfanyia hivyo.
Licha
ya hujuma alizopewa ambazo zinasadikika kuwa za kisiasa mbunge wa viti
maalumu kupitia chama cha demokrasia na maendeleo chadema CHIKU ABWAO
aliendelea na zoezi lake la kutoa msaada wa shilingi milioni moja ili
kusaidia majukumu mengine ya shule hiyo kutokana tathimini fupi
iliyotewa na baadhi ya walimu.
Akizungumza
mbele ya wanafunzi wa shule CHIKU ABWAO amesema kuwa ameguswa na
ajali hiyo ya moto ndio maana ameamua kujitolea kutoa msaada huo.
aidha
ABWAO ameishauri serikali kujenga mabweni kwa mtindo nyumba za kawaida
ili kuwawezesha wanafunzi kuishi kumi katika bweni moja tofauti na sasa
ambapo wanafunzi wanaishi zaidi ya mia na ishirini katika bweni moja.
Lakini
ABWAO akasisitiza kuweka ulinzi mzuri kwenye mabweni kwa kuwa suala
kama hilo limekuwa likijitokeza mara kwa mara katika shule hiyo na
kuomba wakandarasi watakao kuwa wanapewa tenda za kujenga mabweni ya
shule kuhakikisha wanaweka vifaa maalum vya kuzimia moto.
Alipotafuta
mkuu wa shule kwa njia ya simu na kuulizwa kwanini umemkimbia mbunge
alijibu kwa kusema kuwa alikuwa na majukumu mengine kwa hiyo sio lazima
kumpokea mbunge wakati kuna majukumu mengine makubwa zaidi ya yeye.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269