Mwanamke
mmoja nchini Marekani amejifungua mtoto mwenye uzito wa paundi 14.1
sawa na kilo 6.4kg na sasa mtoto huyo anakula mara mbili zaidi ya uwezo
wa mtoto mchanga .
BiMaxxzandra
Ford amepata mtoto aliyempa jina Avery, ndiye mtoto mkubwa na mzito
kuwahi kuzaliwa katika hospitali ya wanawake ya mtakatifu Joseph iliyoko
Tampa, Florida.Avery, alizaliwa kwa njia ya kawaida .
Ford
alikuwa hajatanabahi kuwa yu mjamzito mpaka alipotimiza wiki 35 .lakini
mara baada ya kuwa anaongezeka uzito kupita kiasi ,madaktari
wakamthibitishia kuwa yu mja mzito,na kutokana na kasi ya unenepaji
mwanzo Bi Ford alihisi atajifungua watoto pacha,kumbe sivyo.
Debbie
Moore, mkunga katika hospitali hiyo, wasingemruhusu mwanamke huyo
ajifungue kwa njia ya kawaida kama wangegundua mapema ana mtoto mwenye
kilo nyingi kiasi hicho .
Avery
anabaki hospitalini chini ya uangalizi maalumu tangu alipozaliwa tarehe
29 January , lakini anatarajiwa kuruhusiwa kwenda nyumbani hivi
karibuni .
Bi Ford, anaye mtoto mmoja mwenye umri wa mwaka mmoja na mtoto wa kike mwenye miaka mitano.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269