Wananchi na wanafunzi wa shule ya sekondari Idodi Iringa wakishiriki kuzima moto katika bweni la wanafunzi wa kike shuleni hapo amnbalo lilikuwa likiwaka moto leo asubuhi |
MOTO
mkubwa ambao chanzo chake kinatajwa kuwa ni hitirafu ya umeme
umeteketeza bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Idodi
wilaya ya Iringa mkoani Iringa .
Tukio hilo limetokea muda wa saa 4 asubuhi leo wakati
wanafunzi wakiwa wakiwa madarasani wakiendelea na masomo.
Akizungumzia tukio hilo,kamanda wa jeshi la Zimamoto Mkoani Iringa, Inspekta
Kennedy Komba alisema kuwa bweni hilo limeteketea lote na kuunguza mali
zilizoko katika bweni hilo na chache kuokolewa na wananchi waliowahi
kufika eneo la tukio kusaidia kuzima moto huo.
Alisema kuwa chanzo cha moto huo imesababishwa na
hitalafu ya umeme na hakuna mwanafunzi yoyote aliyejeruhiwa na moto huo. Komba
alisema kuwa baada ya jeshi la zimamoto kupata taarifa waliondoka mjini
Iringa ambapo ni zaidi ya kilometa 20 hadi ilipo shule hiyo ili kwenda kuzima moto huo.
Hata hivyo aliwapongeza
wananchi kwa moyo wa ushujaa kujitolea kuzima moto huo na kuwataka
kutoa taarifa mapema pindi majanga ya moto yanapojitokeza katika maeneo
yanayowazungu.
“Endapo tungepata taarifa mapema nina amini
tungeweza kuokoa vitu vingi zaidi na kuwataka wananchi wasitegemee
mtendaji au kiongozi apige simu katika kikosi cha kuzima moto kwani kila
mtu ana haki ya kupiga simu 111 katika kitengo cha mawasiliano cha
jeshi hilo kuweza kutoa taarifa ya majanga, tumetumia muda mdogo kufika
eneo la tukio kutokana ubora wa gari hivyo nawashukuru sana wananchi
kwa taarifa na kuweza kuonyesha ushirikiano katika uzimaji wa moto huo
usilete madhara zaidi “ alisema
Akizungumzia hasara iliyosababishwa ni kiasi gani Komba alisema hadi sasa hawajapata tathmini kamili ya mali zilizoteketea ila baada ya kazi kukamilika itafahamika ni thamani ya vitu vilivyoungua na kuwekwa wazi kwa wanachi.
Akizungumzia hasara iliyosababishwa ni kiasi gani Komba alisema hadi sasa hawajapata tathmini kamili ya mali zilizoteketea ila baada ya kazi kukamilika itafahamika ni thamani ya vitu vilivyoungua na kuwekwa wazi kwa wanachi.
Mbunge wa jimbo la Isimani Wiliam Lukuvi ambako maafa hayo yametokea mbali
ya kuwapa pole walimu na wananchi wa Idodi kwa tukio hilo
bado aliwapongeza wananchi kwa umoja wao kwa kufika mapema
kuthibiti moto huo pamoja na kikosi cha Zimamoto kutoka mjini
Tukio hilo kubwa kulikumba jimbo la Isimani linaloongozwa na mbunge wake Wiliam Lukuvi ambae ni waziri wa nyumba na ardhi
Akizungumza kwa niaba ya mbunge Lukuvi katibu wa mbunge huyo Thom Malenga
alisema kuwa wananchi wamefanyajitihada kubwa katika kuthibiti
moto huo na kuwa mbali ya mali za wanafunzi hakuna madhara kwa binadamu.Kuhusu
thamani ya mali zilizoteketea kwa moto huo alisema kwa sasa bado mapema kujua ila uongozi wa shule hiyo pamoja na wazazi na
wananchi wa Idodi wapo katika kikao ili kujua madhara zaidi na hasara iliyojitokeza.
Agosti 25/ 2009 jumla ya wanafunzi 13 walipoteza maisha baada ya bweni
hilo kuteketea kwa moto na baadhi yao kujeruhiwa kwa ajali kama hiyo ya moto ambayo kwa kipindi hicho moto huo ulisababishwa na shumaa.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269