Mpaka February 12 idadi ya miili ya marehemu waliofariki na kupatikana kwenye ajali ya ndege ya TransAsia Airlines GE235
ambayo ilianguka muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege
Taipei ilikuwa ni maiti za watu 42, pamoja na majeruhi 15 huku kukiwa na
taarifa kwamba mwili wa mtu mmoja bado haujapatikana.
Leo vikosi vya uokoaji vimefanikiwa kuupata mwili wa mtu mmoja ambao haukuwa umepatikana mpaka jana.
Ndege
hiyo ilipata hitilafu kwenye engine moja na kufanya ndege hiyo kupoteza
mwelekeo, ikagonga ukingo wa daraja na kuanguka mtoni.
Siku
ya juzi ndugu wa marehemu walikaa kikao na uongozi wa Kampuni hiyo ya
ndege na kukataa kulipwa fidia ya pesa ambayo ni sawa na jumla ya dola
milioni 14.9 za Taiwan (zaidi ya Ths. Milioni 850/-) ambayo wangepatiwa
ndugu hao kwa kila mtu mmoja aliyefariki kwenye ajali hiyo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269