Mwimbaji
mahiri wa muziki wa Taarab nchini ambaye pia ni mkurugenzi wa kundi la
Jahazi Modern Taarabu,Mzee Yusuph anatarajia kuoa tena mke wa tatu hivi
karibuni huku wake zake wawili wakiwa kwenye bifu zito wakitupiana
vijembe mtandaoni.
Akipiga
stori na Uheard na Soudy Brown alisema kuwa anatarajia kuoa mke huyo
ambaye anaishi huko visiwani Pemba,na kwamba mipango ikiwa tayari kila
kitu kitakuwa hadharani.
Hivi
karibuni wake zake wawili ambao ni Malkia Leila Rashid ambaye pia ni
mwimbaji wa kundi hilo na mke wake mdogo aitwaye Chiku wamekuwa
wakirushiana vijembe kwenye mtandao wa kijamii wa ‘WathsAAp’ kwa
kuandikiana ‘Status’ za vijembe.
Mzee Yusuph akiwa na mke wake pili,Chiku.
Habari
zinasema kuwa wake hao wamekuwa kama chui na paka na mzee Yusuph hana
mpango wa kuwapatanisha kwa kuwa hakuna hata mmoja aliyeonyesha chuki
kwa mwenzake akiwa na nao.
‘’Waache
tu warushiane vijembe tena ndiyo vizuri na dawa yao nawaletea mke wa
tatu na wala sina mpango wa kuwapatanisha,’alisema Mzee Yusuph
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269