Mtu mmoja
amefariki dunia na wengine 19 kujeruhiwa katika manispaa ya
Kigoma-Ujiji mkoani Kigoma baada ya kutokea ajari ya gari aina ya hiace
iliyokuwa ikiikwepa gari ndogo aina ya Noah bila mafanikio na kuingia
kwenye mtalo huku ikiigonga gari ile ndogo kwa nyuma.
Ajari
hiyo ilitokea jana majira ya saa nane mchana maeneo ya Mlole sabasaba
baada ya hiace lililokuwa likielekea kijiji cha Msimba Wilaya ya Kigoma
vijijini na kabla haijatoka nje ya mji ndipo gari dogo aina ya Noah
ilikuwa ikingia barabara kuu hivyo katika jitihada za dereva wa Hiace
kutaka kulikwepa akajikuta akiingia kwenye mtalo hata hivyo aliigonga
noah kwa nyuma.
Baada
ya ajari hiyo Dereva wa Noah iliyogongwa alifariki dunia huku abiria 19
waliokuwa kwenye Hiace walijeruhiwa na kufikishwa katika hospitali ya
mkoa Maweni kwaajiri ya matibabu.
Kibonajoro ilifika
katika hospitali hiyo ili kuongea na majeruhi kwa lengo la kujua hari
zao na nini chanzo cha ajari hiyo ambapo, Jamali Adamu ambaye ni konda
wa Hiace lile, alisema kuwa awali aliona gari dogo likiingia barabarani
ndipo dereva wa hiace alipojaribu kulikwepa wakajikuta wakiangukia
kwenye mtalo.
Adamu aliiambia Kibonajoro kuwa
baada ya kuanguka alikuwa hajiwezi ila aliona watu wakimbeba kwenye
mabega na kumweka kwenye gari ambapo alipelekwa moja kwa moja
Hospilalini kwaajiri ya matibabu kwani aliumia sehemu ya chini ya mdomo
huku akijisikia maumivu kichwani.
Aidha
Asha Deo alisema kuwa wakati wakiwa kwenye safari dereva alikuwa
akiendesha gari kwa kasi japo abiria walimwambia apunguze mwendo ila
hakupunguza ndipo ilipotokea gari nyingine na kutaka kuigonga akapeleka
gari kwenye mtalo.
“Ajari
hii ni sababu ya mwendo kasi kwani kama dereva angesikia alivyokuwa
akiambiwa na abiria tusingepata ajari, lakini alipoambiwa yeye
alituuliza kuwa hamtaki kuwahi kufika, huku akiendelea kuongeza mwendo” alisema Deo.
Pia
Ahmad Samweli ambaye ni mkazi wa Msimba alisema kuwa walipoanza safari
gari lilikuwa katika mwendo huku Hiace walilopanda lilikuwa likifukuzana
na gari lingine ila hawakujua kinachoendelea nje kwani walikua viti vya
nyuma ndipo wakasikia mshindo mkubwa na kushitukia wako mtaloni.
Nae
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa Maweni, Fadhiri Kibaya
alisema kuwa baada ya ajari hiyo walipokea majeruhi 19 na mtu mmoja
aliyekuwa ameshafariki alifikishwa moja kwa moja mochwari.
“Katika
idadi hiyo ya majeruhi wanaume wako 9 na wanawake 9 huku akiwemo mtoto
mdogo aliyekuwa amebebwa na mama yake kabla ya ajari na wote hao wako
wodini kwaajiri ya matibabu ila mwili wa marehemu unasubilia ndugu zake
kwaajiri ya taratibu za mazishi” alisema Kibaya.
Hata
hivyo Kibaya alisema kuwa yupo mgonjwa mmoja ambaye ni mahututi ambaye
alichomwa na chuma kwenye paji la uso na kikabaki palepele usoni hivyo
yuko chumba cha upasuaji kwaajiri ili kuondolewaa chuma hicho.
Kwa
upande wake Kamanda wa Polisi Mkoani Hapa, Kamishina Msaidizi ACP,
Japhar Muhamed alithibitisha kutokea kwa ajari hiyo na taratibu za
uchunguzi zinafanyika ili kupata taarifa kamili.
Chanzo..Emmanuel Senny Kigoma.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269