Breaking News

Your Ad Spot

Feb 15, 2015

WATANZANIA WAPOKEA TUZO YA MAONYESHO YA SANAA MUSCAT



fakh1. Naibu Balozi wa Tanzania nchini Oman Juma Othaman mwenye Kaunda suti akipokea Tunzo ya ushiriki iliyotolewa na Mwakilishi kutoka Manispaa ya Mji wa Muscat ambao ni Waandaaji wa Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni. Tanzania imepeleka zaidi ya Watu 40 kuonesha kazi wanazoifanya za sanaa ikiwemo,Uchongaji,uchoraji na ufumaji wa nguo. Kulia ni Kiongozi wa Msafara huo Khadija Battashy na kushoto ni Msaidizi kiongozi Masha Hussein. Picha na Faki Mjaka, Muscat Oman fakh2Naibu Balozi wa Tanzania nchini Oman Juma Othman katikati akiwa kashika Tunzo ya ushiriki wa Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni nchini Oman waliyopewa kutoka Manispaa ya Mji wa Muscat ambao ndio waandaaji wa Maonesho hayo. Kulia kwake ni Kiongozi wa Msafara wa Washiriki kutoka Tanzania Khadija Battashy na kushoto ni Msaidizi kiongozi Masha Hussein na Mkuu wa mambo ya kiufundi wa Msafara Moza Habib.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages