Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Magereza, John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha
Mgeni rasmi kufunga Mafunzo ya Uongozi Daraja la Pili kwa Maafisa wa
Jeshi la Magereza.
(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,
IGP Ernest Mangu akipokea Salaam ya heshima kutoka kwa Gwaride
lililoandaliwa na Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi Daraja la Pili(kushoto
katika Jukwaa) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir
Minja.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,
IGP Ernest Mangu akikagua Gwaride Maalum lililoandaliwa na Wahitimu wa
Mafunzo ya Uongozi wa Magereza Daraja la Pili ambayo yamefungwa rasmi
leo Juni 22, 2015 katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es
Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Magereza, John Casmir Minja (kulia) akifurahia onesho Maalum la Maafisa
wa Jeshi la Magereza kutoka Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani
(katikati) ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu
(kushoto) ni Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylivester Ambokile
wakifurahia onesho hilo kama wanavyoonekana katika picha.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa umakini
matukio mbalimbali katika sherehe hizo za kufunga Mafunzo ya Uongozi
Daraja la Pili(wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa
Magereza, Dkt. Juma Malewa(katikati) ni Kamishna wa Huduma za
Urekebishaji, Deonice Chamulesile(kulia) ni Mkuu wa Chuo cha Maafisa
Magereza Ukonga, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Erasmus Kundy.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,
IGP Ernest Mangu akimvisha cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Magereza Mhitimu
wa Mafunzo ya Uongozi wa Magereza Daraja la Pili ambaye amefanya vizuri
kwa upande wa Gwaride, Stafu Sajini Boniphace Felix. Mhitimu huyo
amevishwa cheo hicho kwa niaba ya Wahitimu 216 wa Mafunzo hayo.
Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi
wa Magereza Daraja la Pili wakipita mbele ya Mgeni rasmi IGP Ernest
Mangu (hayupo pichani), katika mwendo wa haraka wakitoa heshima leo Juni
22, 2015 katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga. Jumla ya Wahitimu 216
wamehitimu Mafunzo Uongozi Daraja la Pili na kupandishwa cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Magereza.
Maafisa wa Jeshi la Magereza
wakionyesha umahiri mkubwa wa mbinu mbalimbali za kujihami na adui kama
wanavyoonekana kikakamavu katika picha wakati wa hafla fupi ya kufunga
Mafunzo ya Uongozi Daraja la Pili.
Kikundi cha kwaya kinachoundwa na
Maafisa wa Jeshi la Magereza wa Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga
kikitumbuza mbele ya Mgeni rasmi, IGP Ernest Mangu(hayupo pichani)katika
sherehe za kufunga Mafunzo hayo ya Uongozi Daraja la Pili, Chuo cha
Maafisa Magereza Ukonga.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269