Breaking News

Your Ad Spot

Jun 22, 2015

KINANA ACHAPA KAZI JIMBO LA SENGEREMA LEO, AKAGUA MIRADI KADHAA NA KUZINDUA KIVUKO CHA KISASA CHA KAMANGA, MKUTANO SENGEREMA MJINI 'WATAPIKA' MAELFU YA WANANCHI KUMSILIKIZA

 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwasili kuhutubia mkutano wa hadhara aliofanya katika Viwanja vya CCM, wilaya ya Sengerema mjini, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM na Uhai wa Chama mkoani Mwanza, leo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara aliofanya katika viwanja vya Ofisi ya CCM, wilaya ya Sengerema mjini, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama mkoani Mwanza leo
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akuhutubia mkutano wa hadhara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana uliofanyika leo na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi, katika viwanja vya CCM wilaya ya Sengerema mjini.
 Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja, akieleza alivyoshiriki katika utekelezaji wa ilani ya CCM, alipohutubia mkutano wa katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi katika Viwanja vya Ofisi ya CCM wilaya ya Sengerema mjini leo.jioni
 Wananchi waliofurika katika Uwanja wa Ofsi ya CCM wilaya ya Sengerema mjini, wakishangilia wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CM Abdulrahman Kinana uliofanyika kwenye viwanja hivyo leo jioni
 Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana uliofanyika leo kwenye viwanja vya CCM wilaya ya Sengerema mjini.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiteta jamb na Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo wakati wa mkutano wake wa hadhara uliofanyika leo katika Viwanja vya Ofisi ya CCM wilaya ya Sengerema mjini.
 "Naam mkutano wetu umefanikiwa" inaelekea ndivyo alivyokuwa akiwaza huku akitabasamu, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati wa mkutano wake wa hadhara aliofanya leo, kwenye Viwanja vya CCM wilaya ya Sengerema mjini.

ALIPOKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KABLA YA MKUTANO HUO
 "Kwa hiyo mradi huu ndiyo umekwamia palee, siyo", Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimuuliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Mathew Lubongeja, alipokagua mradi wa Kilimo cha Skimu, Katunguru, alipokagua mradi huo akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama, katika Jimbo la Sengerema mkoani Mwanza. Mradi huo ambao ni mkubwa umekwama kumalizika kwa madai ya kukosa fedha baada ya kutumia sh. milioni 700 tu, kati ya Shilingi Bilioni 2 zilizokuwa zimekadiriwa kumaliza mradi huo. Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, fedha hizo zinatakiwa kutolewa na serikali.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia), na msafara wake wakipita kwenye moja ya matuta ya mradi huo ambao umekwama kumalizika.
 Risala aliyosomewa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wakati alipokagua mradi huo.


 AKIKAGUA SOKO LA HALMASHAURI YA SENGEREMA

 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akikagua hali ya Soko Kuu la Halmashauri ya mji wa Sengerema, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama mkoani Mwanza leo. Soko hilo limelalamikiwa na watumiaji kuwa na uchafu uliokithiri katika maeneo mbalimbali vikiwemo vyoo.
 Vijana wakimuonyesha Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana hali ilivyo mbaya katika moja ya mabucha kutokana na jengo kwenye soko hilo  kuvuja nyakati za mvua
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akitazama mtaro wa maji taka kwenye soko hilo
 Moja ya vyoo vya kulipia katika soko hilo kikiwa na tangazo lilibandikwa katika mtindo wa aina yake.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana aitazama maji machafu yanavyotiririka hovyo kutoka kwenye vyoo
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimhoji Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja kujua imekuwaje hadi hali ya soko kuwa mbaya, alipokagua vyoo na kushuhudia hali mbaya

UHAI WA CHAMA.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza katika Kikao Cha Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Sengerema, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama mkoani Mwanza leo
MRADI WA KIVUKO
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa kwenye Kivuko cha Sumar III, alipozindua kivuko hicho kinachoendeshwa na mwekezaji, kwenye eneo la Kamanga, leo, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCm na uhai wa Chama wilayani sengerema mkoani Mwanza. Kivuko hicho kinaunganisha Sengerema na Mwanza mjini.
 Kinana akizungumza na wananchi baada ya kukagua kivuko hicho
 Mbunge wa Sengerema, william Ngeleja akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kivuko hicho leo
 Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo akizungumza wakati wa kuzinduzi wa kivuko hicho
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wakienda kuingia kwenye Kivuko hicho kabla ya uzinduzi
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akikata utepe kuzindua Kivuko hicho
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisaini kitabu baada ya kuzindua kivuko hicho
 Taswira ya kivuko hicho cha Kisasa
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman kinana akizindua jiwe la msingi ujenzi wa Ofisi ya CCM wilaya ya Sengerema akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama mkoani Mwanza
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akikagua ujenzi tangi na chujio la maji la  mradi wa maji wa Sengerema mjini uliopo eneo la Nyamazugowa, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama mkoani Mwanza, leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO-CCM Blog

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages