Naibu Katibu Mkuu,Ofisi ya Makamu
wa Rais Mhandisi Angelina Madete akiwaeleza waandishi wa Habari (hawapo
pichani) kuhusu mafanikio ya serikali ya nne ikiwamo kujenga umoja,
amani na utulivu miongoni mwa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari
(MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara
ya Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi.
Picha na Hassan Silayo-MAELEZO
Mkurugenzi wa Muungano, Ofisi ya
Makamu wa Rais Bw. Baraka Rajab Baraka akitoa wito kwa wananchi kulinda,
kuudumisha na kuendeleza muungano ili kuwa na nchi yenye umoja, amani
na usalama, wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya
Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Naibu Katibu
Mkuu,Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Angelina Madete.
Kaimu Mkurugenzi Uzingatiaji na
Ufuatiliaji wa Sheria kutoka Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) Ruth
Lugwisha akiwaasa wananchi kubadili tabia na kuacha kutumia mifuko ya
plastiki isiyoruhusiwa ili kuepuka uchafuzi wa Mazingira na Athari zake,
wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari
(MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara
ya Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi.
…………………………………………….
Na Frank Mvungi-MAELEZO
Serikali imeendelea kuimarisha umoja,amani na utulivu miongoni
mwa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kipindi cha miaka
kumi.
Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais
Mhandisi Angelina Madete wakati wa mkutano na vyombo vya habari leo
jijini Dar es salaam.
Mhandishi Madete alisema kuwa suala la muungano ni miongoni mwa
vipaumbele vya Serikali ya awamu ya nne kwa dhumuni la kuimarisha umoja
na utulivu nchini.
“Serikali ya awamu ya nne inajivunia uimarikaji wa Umoja, amani
na utulivu miongoni mwa wananchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kwani ilikuwa ni moja ya kipaumbele kilichowekwa na serikali hii katika
kipindi cha miaka Kumi ya Uongozi wa Rais Dkt. Jakaya Kikwete.” Alisema
Mhandisi Madete.
Mhandishi Madete aliongeza kuwa Taasisi za Muungano kama Ulinzi
na Usalama,Uhamiaji na Uraia,Fedha , Sarafu na Mawasiliano zimeendelea
kuimarika kwa kutoa huduma bora kwa wananchi katika kipindi cha Serikali
ya awamu ya nne.
Akifafanua Madete amesema katika kipindi cha awamu ya nne
wananchi wa pande zote mbili za muungano wameendelea kunufaika na
shughuli za kiuchumi na kuongeza ajira kupitia utekelezaji wa program za
maendeleo ikiwemo mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF),Progamu ya
usimamizi wa Bahari na Pwani (MACEMP) na mradi wa kutoa mikopo kwa ajili
ya miradi midogomidogo (SELF).
Miradi mingine ni program ya maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
, mradi shirikishi wa program za maendeleo ya kilimo( PADEP) na program
yamaendeleo ya Mileninia ambayo kwa pamoja imewanufaisha wananchi kwa
kuwaletea maendeleo endelevu.
Mafanikio mengine ni ujenzi wa majengo ya Taasisi za Muungano
ikiwemo kukamilika kwa ujenzi wa Ofisi ya Makamu wa Rais,Mtaa wa
Lithuli,Dar es salaam,awamu ya pili ya ujenzi wa ofisi ya Makamu wa Rais
Tunguu-Zanzibar umekamilika kwa kiwango kikubwa.
Pia ujenzi wa Tawi la Benki Kuu lililopo Gulioni Zanzaibar
umekamilika ambapo majengo mengine yaliyojengwa ni pamoja na
uhamiaji,Makao makuu na Ofisi za BungeTunguu na Tume ya Sayansi na
Teknolojia (COSTECH).
Ofisi ya Makamu wa Rais itaendelea kuratibu shughuli za Muungano
na kudumisha ushirikiano kati ya Serikali ya Muungano na Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar na Pia itaendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu
wa Muungano kwa wananchi wote.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269