Na Mwandishi Wetu
MAHAKAMA
ya Mwanzo Kizuiani Mbagala Jijini Dar es Salaam, kesho, Oktoba 25
inatarajia kutoa hukumu kwenye kesi ya madai ya talaka na mgawanyo wa
mali iliyofunguliwa na mkazi wa Singida, Magreth Mwangu dhidi ya
Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya St. Mathew na St. Marks,Thadei
Mtembei.
Katika
madai yake ya Msingi, Mwangu anaomba mahakama imuamuru mdaiwa kutoa Sh.
Milioni 800 na makazi ya kukaa mdai na watoto wake.
Kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu Rajab Tamaambele.
Miongoni
mwa mashahidi waliotoa ushahidi mahakamani hapo ni pamoja na Mwangu
ambaye alidai kuwa alianza kuishi na Mutembei mwaka 1995 Kongowe Mbagala
ambapo mwaka 1998 alikwenda kwa wazazi wa Mwangu kijiji cha Kwaye
Iguguno Singida ambapo alitoa mahali na walifunga ndoa ya kimila.
Alisema mtoto wa kwanza alizaliwa mwaka 1998, huku mtoto wa pili akizaliwa mwaka 2000 na mtoto wa tatu 2003
Katika
ushahidi wao, watoto wa Mwangu ambao wanasoma katika shule za St Mary’s
International na Hijra Seminari ya Dodoma, wamedai kuwa wanasumbuliwa
ada na kwamba wanahitaji malezi yote kutoka kwa baba yao.
Watoto hao waliiambia mahakama kuwa, mara ya mwisho kumuona baba yao ni mwaka 2011.
Mtoto
wa kwanza wa Mwangu alidai kuwa mwaka 2012 walifika katika Hoteli ya
baba yao ya Sleep inn ndipo aliwafukuza na kuwaambia kuwa hawezi
kuwalipia ada na badala yake aliwapa Sh 40,000 kila mmoja, fedha ambazo
aliziacha mezani.
Pia
walidai kuwa Mtembei aliwatolea maneno ya kashfa kwamba hata mama yao
aende wapi, anao uwezo na kwamba anajeshi ambalo popote linafika.
Wakati wa ushahidi wake Mutembei alisema alifahamiana na Mwangu wakati akiwa na mfanya usafi katika duka lake la dawa.
Alisema hakuwahi kumuoa mama huyo wala kuishi naye licha ya kuzaa naye watoto watatu.
KAWAIDA
court_gavel
Na
Mwandishi Wetu
MAHAKAMA ya Mwanzo Kizuiani Mbagala Jijini Dar es Salaam, kesho, Oktoba
25 inatarajia kutoa hukumu kwenye kesi ya madai ya talaka na mgawanyo wa
mali iliyofunguliwa na mkazi wa Singida, Magreth Mwangu dhidi ya
Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya St. Mathew na St. Marks,Thadei
Mtembei.
Katika madai yake ya Msingi, Mwangu anaomba mahakama imuamuru mdaiwa
kutoa Sh. Milioni 800 na makazi ya kukaa mdai na watoto wake.
Kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu Rajab Tamaambele.
Miongoni mwa mashahidi waliotoa ushahidi mahakamani hapo ni pamoja na
Mwangu ambaye alidai kuwa alianza kuishi na Mutembei mwaka 1995 Kongowe
Mbagala ambapo mwaka 1998 alikwenda kwa wazazi wa Mwangu kijiji cha
Kwaye Iguguno Singida ambapo alitoa mahali na walifunga ndoa ya kimila.
Alisema mtoto wa kwanza alizaliwa mwaka 1998, huku mtoto wa pili
akizaliwa mwaka 2000 na mtoto wa tatu 2003
Katika ushahidi wao, watoto wa Mwangu ambao wanasoma katika shule za St
Mary’s International na Hijra Seminari ya Dodoma, wamedai kuwa
wanasumbuliwa ada na kwamba wanahitaji malezi yote kutoka kwa baba yao.
Watoto hao waliiambia mahakama kuwa, mara ya mwisho kumuona baba yao ni
mwaka 2011.
Mtoto wa kwanza wa Mwangu alidai kuwa mwaka 2012 walifika katika Hoteli
ya baba yao ya Sleep inn ndipo aliwafukuza na kuwaambia kuwa hawezi
kuwalipia ada na badala yake aliwapa Sh 40,000 kila mmoja, fedha ambazo
aliziacha mezani.
Pia walidai kuwa Mtembei aliwatolea maneno ya kashfa kwamba hata mama
yao aende wapi, anao uwezo na kwamba anajeshi ambalo popote linafika.
Wakati wa ushahidi wake Mutembei alisema alifahamiana na Mwangu wakati
akiwa na mfanya usafi katika duka lake la dawa.
Alisema hakuwahi kumuoa mama huyo wala kuishi naye licha ya kuzaa naye
watoto watatu.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269