Mufti
Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi wakwanza kushoto akitoa maelezo
juuya haki za binaadamu kwa mujibu wa Uislam wakati alipokuwa
akifunguwa Mafunzo ya Haki za Binaadamu na kuwatambulisha wasaidizi wa
Sheria kwa Viongozi wa Dini, katikati ni Mkurugenzi Mtendaji Harusi
Miraji na mwisho Jina Mwinyi Waziri Afisa Mipango wa Kituo cha Huduma na
Sheria.
Sheikh
Thabit Nooman Jongo kutoka Afisi ya Mufti Zanzibar akiwafahamisha jambo
washiriki wa mafunzo ya Haki za Binaadamu katika Ukumbi wa Mazsons Hotel
mjini Zanzibar
Na Miza Othman –Maelezo Zanzibar 26/08/2015.
Mashekhe
na Walimu wa Madrasa wametakiwa kuwashajihisha Wananchi ili waepuke
kujiingiza katika makundi yanayoweza kuvunja amani katika kipindi hiki
cha Mchakato wa Uchaguzi Mkuu nchini.
Hayo
yameelezwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi alipokuwa
akifunguwa mafunzo ya Haki za Binaadamu yaliyoandaliwa na Kituo cha
Huduma za Sheria Zanzibar na kufanyika katika ukumbi wa Mazsons
Hotel,Shangani Mjini Zanzibar.
Amesema
Masheikh na Walimu hao ndio Wasimamizi wakuu katika maeneo mbalimbali
ikiwemo Miskitini, Madrasani na hata ndani ya Nyumba zao kwani kufanya
hivyo kutawasaidia kuepuka Uvunjifu wa Amani ni.
“Tofauti
za dini, jinsia, cheo na Kabila sio njia za ukiukwaji wa Sheria ndani ya
Nchi yetu bali zitumike katika kutii sharia kwa kila raia”,alisema
Shekh Kaabi.
Nae Shekh
Thabit Nooman Jongo kutoka Afisi ya Mufti Zanzibar amewataka Walimu na
Mashekhe wenzake kuwa mstari wa mbele katika kusimamia juu ya ukumbusho
huo kwani kufanya hivyo ni kutekelaza majukumu yao.
Aidha
amewataka Masheikhe na Walimu hao kuchukuwa juhudi za hali ya juu na
kutumia maneno ya hekima, busara na unyenyekevu ili waweze kufanikiwa
malengo waliyokusudia.
Hata
hivyo amesema kuwa wakati wanapotoa hutuba zao ndani ya Misikiti na
Madrasa ziwe ni zenye kujenga amani kwani kufanya hivyo ni kuzitii
sheria zilizowekwa katika nchi yao.
Kwa
upande wao Washiriki wa mafunzo hayo wamesema watayafanyia kazi bila ya
kinyongo na kuyafikisha katika maeneo yao kama walivyoagizwa na Viongozi
wenzao.
IMETOLEW NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269