Ofisa
Mradi wa mpango wa kutekeleza mkakati wa kupunguza vifo vinavyotokana
na ajali za barabarani kwa kusisitiza usalama Barabarani unaosimamiwa
kwa kushirikiana na Bloomberg (BIGRS), Shirika la afya Duniani (WHO)
na Serikali ya Tanzania, Mary Kessi (katikati), akitoa mada kwenye
semina hiyo iliyowajumuisha wanahabari na wadau wa sekta ya usafiri
inayohusu mpango huo wa utekelezaji wa mkakati huo.
Mtaalamu Mwelekezi, Callie Long kutoka Canada akitoa mada kwenye semina hiyo.
Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo, Asah Mwambene akitoa mada kwenye semina hiyo.
Mwanasheria
wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Mkaguzi wa Polisi Sokoni Deus
(katikati), akitoa mada kwenye semina ya siku mbili ya wanahabari na
wadau wa sekta ya usafiri Dar es Salaam leo asubuhi, inayohusu mpango
wa kutekeleza mkakati wa kupunguza vifo vinavyotokana na ajali za
barabarani kwa kusisitiza usalama Barabarani.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye
semina hiyo.
Semina ikiendelea.
Mmoja wa wadau wa semina hiyo akichangia jambo.
Na Dotto Mwaibale
Mradi
wa usalama barabarani kwa kushirikiana na Bloomberg (BIGRS), Shirika
la afya Duniani (WHO) na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya na
Ustawi wa umeanza kutoa mafunzo kdau wa sekta wa usafiri wakiwemo
wanahari, wanasheria kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya ajali.
Akizungumza
Dar es salaam leo kwenye semina ya siku mbili inayohusu mpango wa
kutekeleza mkakati wa kupunguza vifo vinavyotokana na ajali za
barabarani kwa kusisitiza usalama Barabarani, Ofisa Mradi huo, Mary
Kessi alisema waandishi wamekuwa wakisubiri matukio ya ajali ndipo
waripoti habari hizo jambo ambalo si lazima lisubiriwe na inachotakiwa
ni kujenga mazoea ya kuandika habari za kufundisha jamii na watumiaji wa
vyombo vya moto namna ya kuweza kuepuka kusababisha ajali.
"Dhumuni
la semina hii ni kujua jinsi ya kuripoti habari hizi za usalama
barabarani ili kufikia walengwa kwa kuongea kupitia vyombo vyenu vya
habari ili kuwapa ulewa watu wote' alisema Kessi.
Alisema
kuwa mpango huo wa miaka mitano utaelekeza katika kupunguza ajali za
barabarani huku takwimu zinaonyesha ajali hizo zimekuwa zikiua watu
milioni1.24 kila mwaka Duniani, kitu ambacho kinarudisha nyuma maendeleo
ya taifa huku kati ya hao 20 upata ulemavu kutokana na ajali.
Alifafanua
kuwa uzembe wa madereva usababisha ajali zinazoweza kuzuilika na
kuzitaja sababu hizo kuu ni kutofunga mikanda ,kuendesha gari kwa kasi
,matumizi ya pombe kupita kiwango na kutoweka vizuwizi vya watoto.
"Uendeshaji
wa gari ukiwa umelewa ni kitu kibaya sana wengine wanaendesha gari huu
wanachati na simu bila kujali kilichokua mbele wala nyuma yake"alisema
Daktari
wa Kitengo cha Maafa na Dharura wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
Mery Kitambi,alisema Hospitali za mikoa zilizopo nchini hapa zimejaa
majeruhu wa ajali pamoja na vifo vinavyo sababishwa na ajali hizo.
Alisema
waandishi wanatakiwa kuleta fikra mpya kwa watumia wa vyombo hivyo vya
moto ili wajue ni kiasi gani wanajiweka katika hatari na jinsi ya
kuepuka hatari hizo.
"Ukienda
hospitali utawakuta majeruhi wa ajali ni wengi kuliko unavyo fikiria
hivyo ni vyema wakajua kwa undani jinsi gani ya kuepuka ajali za
kizembe"alisema Kitambi.
Mwanasheria
wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Mkaguzi wa Polisi, Sokoni
Deus, alisema wazazi wanatakiwa kuacha tabia ya kuwapa watoto walio
chini ya miaka 18 kuendesha vyombo vya moto kwani usababisha ajali.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269