CHAMA Cha Mapinduzi leo kimemaliza Kikao chake cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), kilichoanza jana, kufanya kazi ya kuteua wagombea ubunge na uwakilishi katika majimbo yote nchini.
NEC imefanya uteuzi huo, huku
majimbo 11 kati ya 240 yaliyopo nchini ikiwa imeyaweka kiporo cha kusubiri maamuzi yake kutolewa Agosti 17, mwaka huu katika kikao kingine kitakachofanywa na Kamati Kuu Maalum ya CCM.
Kuwekwa kiporo kwa majimbo hayo 11, kumetokana na sababu mbalimbali ikiwemo yaliyolazimika kurudia kura za maoni kutokana na kutokeza kasoro tofauti tofauti.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo baada ya kumalizika kwa kikao cha
halmashauri kuu ya CCM (NEC) katibu wa NEC Itikadi na Uenezi ndugu Nape NNauye amesema vikao vilivyoanza na Kamati ya Usalama na Maadili na Kamati Kuu, vilikuwa virefu lakini vyenye mafanikio makubwa kwa sababu ya kujadili kwa umahiri mkubwa majina 2721 ya wanachama wote walioomba ridhaa ya kugombea Ubunge, Uwakilishi na Viti maalum.
HATIMAYE NAPE ALIWEKA HADHARANI ORODHA YA MAJINA YA AMBAO KUPITIA VIKAO HIVYO CCM IMEWATEUA KUGOMBEA UBUNGE NA UWAKILISHI WA MAJIMBO NA VITI MAALUM KATIKA UCHAGUZI WA OKTOBA, MWAKA 2015
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269