Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida, ACP Thobias Sedoyeka.Vipande viwili vya fuvu la binadamu.Chupa tatu za mafuta ya simba alizokutwa nazo mtuhumiwa.
Vipande vya ngozi ya simba
JESHI la
polisi mkoani Singida linamshikilia mkazi moja wa Kijiji cha Itumba,
wilaya ya Igunga, mkoani Tabora kwa tuhuma za kukutwa na viungo vya
binadamu na nyara za serikali.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida,
ACP Thobias Sedoyeka, amemtaja mtuhumiwa kuwa ni Magida Bundala
aliyekamatwa akitoka mkoani Tabora kuja Singida kusalimia ndugu zake
ambao walikuwa wamewekwa mahabusu katika Kituo cha Polisi cha Wilaya ya
Ikungi.
Kamanda
Sedoyeka alisema walimkamata mtuhumiwa huyo baada ya askari kumtilia
mashaka na kuamua kumkagua wakati akisubiri kuwasalimia ndugu zake ambao
ni mahabusu alipokutwa na vipande viwili vya fuvu la binadamu, ngozi ya
chatu, vipande vya ngozi ya simba, pembe ambayo haijajulikana kuwa ni
ya mnyama gani na chupa tatu za mafuta ya simba.
Wakazi wa
Manispaa ya Singida wameliomba jeshi la polisi kuhakikisha
linamfuatilia mtuhumiwa huyo ili kubaini mtandao mzima kwa sababu
unaendesha shughuli zao kutokana imani potofu ikiwa ni pamoja kupata
madaraka, jambo ambalo husababisha vifo kwa binadamu wakiwemo walemavu
wa ngozi (albino).
CHANZO: ITv
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269