Askari wa Israel akijitayarisha kumpiga risasi msichana mwenye asili ya Palestina, Hadeel al-Hashlamon...Askari wenzake wakimzuia asifanye chochote kwa binti huyo.Hofu ikitanda kwa maaskari hao.Hadeel al-Hashlamon akiwa chini baada ya kupigwa risasi.Maaskari hao wakimkagua Hadeel mara baada ya kumpiga risasi.Mwili wa marehemu Hadeel al-Hashlamon ukipelekwa hospitili kuhifadhiwa.
Mwanafamilia wa Hadeel al-Hashlamon akilia kwa uchungu mara baada kumpoteza nduguye.
Picha
inaonyesha wakati ambapo askari wa Israel mwenye silaha akijitayarisha
kumpiga risasi msichana wa Kipalestina (aliyevaa nikabu) sekunde chache
baada ya msichana huyo kujaribu kumchoma kisu mlinzi wa Israel katika
Ukingo wa Magharibi Magharibi.
Hadeel
al-Hashlamon, mwenye umri wa miaka 18, alipigwa risasi jana katika
Ukingo wa Magharibi baada ya kudorora kwa usalama katika eneo hilo kabla
ya kuadhimishwa kwa sikukuu za Wayahudi na Waislam wiki hii.
Picha
zilizochukuliwa muda mfupi kabla ya msichana huyo kuuawa zinaonyesha
jinsi askari wasiopungua wawili wa Israel walivyokuwa wamemlenga na
bunduki zao kabla ya kuuawa kwake. Jeshi la Israel lilithibitisha mauaji
hayo yaliyotokea katika mji wa Hebron ulio katika Ukingo wa Magharibi.
Msichana
huyo aliyekuwa anasoma chuo kikuu, alikimbizwa katika hospitali moja
nchini Israel akiwa mahututi ambapo baba yake, Salah al-Hashlamon,
alisema baadaye kwamba alifariki kwa majeraha. Askari aliyemuua hakupata
madhara yoyote.
NA DAILYMAILY
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269