Breaking News

Your Ad Spot

Sep 25, 2015

ILI KUDHIHIRISHA UTIMAMU WA AFYA YAKE DK MAGUFULI ARUKA KUTOKA JUU YA GARI KAHAMA


 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akijiandaa kuruka kutoka kwenye gari alipowasili kwenye mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Milango Kumi mjini Kahama.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akipanda ngazi kwenda jukwaani baada ya kuwasili kwenye mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Milango Kumi Mjini Kahama

 Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi mjini Kahama, mkoani Shinyanga leo, ambapo akishinda urais ameahidi kuupandisha mji huo huo kuwa Mkoa,Ili apate ushindi wa kishindo amewataka wananchi kutobweteka na  matokeo ya tafiti zilizotangaza kwa mba atashinda kwa asilimia 65. bali wajitokeze kwa wingi Oktoba 25 mwaka huu kump0igia kura ili apate ushindi wa kishindo.



 Umati wa watu wakimsikiliza kwa makini Dk Magufuli akijinadi katika mkutano wa kampeni mjini Khama leo.

 Wananchi mjini Khama wakionesha dole gumba ikiwa ni ishara ya kukubali kumpigia kura Dk Magufuli siku ya uchaguzi mkuu.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Dk Magufuli akiwahutubia wananchi katika mji wa Nyarugusu katika Jimbo la Busanda mkoani Geita, ambapo aliahidi kuboresha uchimbaji mdogo mdogo wa madini nchini kwa kuwapatia mikopo ya fedha na vifaa vya kuchimbia

 Wananchi wakinyoosha mikono ikiwa ni ishara ya kukubali kumpigia kura za ndiyo siku ya chaguzi mkuu wakiwemp wagombea ubunge na udiwani wa CCM katika Kata ya Nyarugusu, Jimbo la Busanda mkoani Geita.

 Dk Magufuli akimtambulisha kwa wananchi mgombea ubunge Jimbo la Busanda kupitia CCM, Lolensia Butimba katika Mji wa Nyarugusu

 Wananchi wakishangilia wakati msafara wa Dk Magufuli ukiwasili katika Mji wa Bukoli

 Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi katika Mji wa Bukoli

 Mstaafu akionesha bango wakati Dk Magufuli akihutubia katika Mji wa Bukoli ambapo aliahidhi kwamba akishinda serikali yake itaanzisha pensheni kwa wazee nchini

 Mtoto akishangilia baada ya kumuona Dk Magufuli katika Mji wa Bukoli

 Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye jengo la shule walipokuwa wakimsikiliza Dk Magufuli katika mkutano wa kampeni katika Mji wa Ushirombo, wilayani Bukombe, GeitaPICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Wananchi wakimshangilia Dk Magufuli na kukubali kumpigia kura za ndiyo katika Uchaguzi Mkuu

 Dk Magufuli akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Bukombe, Doito Biteko katika mkutano huo

 Wananchi wakisikiliza kwa makini wakati Dk Magufuli akijinadi wilayani Bukombe



 Dk Magufuli akihutubia wananchi na kuwaomba kumpigia kura siku ya uchaguzi

 Wakinyoosha mikono kukubali kumpigia kura Dk Magufuli siku ya uchaguzi Mkuu

 Dk Magufuli akimkabidhi Doto Ilani ya chama hicho



 Dk Magufuli akishangilia na wananchi wa wilaya ya BBukombe

 Wananchi wa Kijiji cha Mabomba wakimshangilia Dk Magufuli

 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mabomba

 Ilibidi wapande juu ya gari ili wapate kumuona vizuri Dk Magufuli alipokuwa akihutubia katika mkutano wa kampeni Jimbo la Ushetu wilayani Kahama

 Wote akinyoosha mikono kukubali kumpigia kura Dk Magufuli jimboni Ushetu

 Dk Magufuli akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho Mgombea ubunge Jimbo la Ushetu, Elias Kuandikwa

 Wapinzania wakirudisha kadi za vyama vyao kwa Dk Magufuli na kutangaza kujiunga na CCM WAKATI WA MKUTANO HUO



 Yamoto Bandi ikitumbuiza wakati wa mkutano wa kampeni za ccm mjini Kahama

 Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM, Samuel Sitta akiwaomba wananchi wa Kahama kumpigia kura Dk Magufuli

Mjumbe wa KIamati ya Kampeni za CCM, Abdallah Bulembo akielezea wasifu wa Dk Magufuli hivyo kuwaomba wananchi wa Kahama kumpigia kura Dk Magufuli katika uchaguzi mkuu ili ashinde urais na kuwaletea neema.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages