Vinara
wa biashara Afrika walipewa tuzo mbalimbali za African Business katika
picha ya pamoja. Kuanzia kushoto ni Daphne Mashile Nkosi, Strive
Masiyiwa, Helen Hai na Mohammed Dewji . hafla ya utoaji wa tuzo hizo
ilifanyika hoteli ya Four Seasons Hotel mjini New York.(Picha na African
Business).
Na Mwandishi wetu, New York
MTANZANIA Bilionea Mohamed Dewji amepata tuzo ya Mfanyabiashara Bora wa Afrika wa mwaka 2015, katika kinyang’anyiro cha tuzo za wafanyabiashara bora wa Afrika (African Business Awards 2015).
Dewji maarufu kama Mo alikabidhiwa tuzo hizo usiku wa kuamkia jana mjini New York.
Katika
hafla hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Four Season mkabala na jengo
la Umoja wa Mataifa (Baraza Kuu) watu wengine waliopata tuzo ni Aliko
Dangote, Daphne Mashile Nkosi, Strive Masiyiwa na Helen Hai.
MO
alimshinda Aliko Dangote ambao walikuwa kwenye Kategori moja wakiwania
tuzo hiyo ya mfanyabiashara bora wa Afrika, huku wengine
walioshindanishwa kwenye kategori hiyo ni CEO wa Paramount Group, Ivor
Ichikowitz, CEO wa Groupe Loukil, Groupe UADH, Bassem Loukil, na Oscar
Onyema DG wa Nigerian Stock Exchange.
Tuzo hizo zimeandaliwa na jarida la African Business .
Pia
katika tuzo hizo taasisi kadhaa zinazofanya vyema bara la Afrika
zilitambulika. Taasisi hizo ni pamoja na kiwanda cha sementi cha Dangote
, Guaranty Trust Bank, Abellon Clean Energy, Nigerian Stock Exchange
na taasisi ya bima kwa masoko yanayochipukia ya BIMA.
Akielezwa
wasifu wake katika hafla hiyo, Mo ameelezwa kama mfanyabiashara
aliyefanikiwa kutokana na kuongeza kipato na ukubwa wa kampuni ya
Mohammed Enterprise toka aitwae kutoka kwa baba yake.
Akiwa
mtendaji wa kampuni hiyo, akiwa katika miaka ya 40 amefanya mabadiliko
makubwa katika makampuni mbalimbali ya umma yaliyoshindwa kujiendesha
katika sekta ya kilimo, viwanda na maeneo ya makazi na viwanda.
Uongozi
wake uliwezesha kampuni hiyo ya MeTL kufanya makubwa kiasi cha kumfanya
aingie katika jarida la Forbes la matajiri wa Afrika.
Majaji waliompa
tuzo kwa mwaka huu walisema kwamba uongozi wake umewezesha biashara
katika kampuni hiyo kuchupa kutoka dola za Marekani milioni 30 hadi
bilioni 3.
Akipokea tuzo hizo
Dewji alisema kwamba tuzo hiyo ni ishara muhimu kwa waafrika wote na
uwakilishi wa uhakika wa vijana katika masuala ya ujasirimali.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji.
Tuzo ya Biashara ya Mwaka ilienda kwa kiwanda cha saruji cha Dangote kinachoongozwa na bilionea wa Afrika, Aliko Dangote.
Kiwanda
hiki kilichopo Nigeria kimejipanga kusambaza uzalishaji katika nchi
nyingine za Afrika, hatua ambayo imeifanya tuzo hiyo kuwa ya kwao.
Akipokea
tuzo hiyo Aliko alisema amefurahishwa sana na tuzo hiyo ya thamani
kubwa na kwamba imetolewa wakati ambapo kiwanda hicho kinatanua shughuli
zake kuhakikisha ukombozi wa uchumi kwa nchi za Afrika unafanyika kwa
dhati.
“Tunaamini
katika Afrika. Tunaamini kwamba katika kuhakikisha kuna uwekezaji
mkubwa wa miundombinu Afrika itaweza kusonga mbele katika uchumi wake”.
Daphne Mashile Nkosi,
Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya manganisi ya Kalagadi ya Afrika
Kusini alipokea tuzo mwanamke bora katika biashara. Majaji walimpa tuzo
hiyo kwa kuwa ameonesha mafanikio makubwa katika sekta ambayo kwa
kawaida huendeshwa na wanaume.
Mdada
huyo anatambulika kwa kuwezesha kupatikana kwa ajira 30,000 huko
Northern Cape, na ni muasisi wa mgodi wa aina yake katika kipindi cha
miaka 30.
Mfanyabiashara wa Zimbabwe, mjasiriamali, anayependa kusaidia watu wenye mahitaji Strive Masiyiwa alipata tuzo ya mafanikio katika maisha.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akipokea tuzo yake.
Strive ambaye ni mmoja wa waanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji kwa kampuni ya kimataifa ya mawasiliano ya simu Econet Wireless amepewa tuzo hiyo kwa mafanikio yake na pia kwa misaada mingi aliyotoa kwa vijana.
Masiyiwa ametumia utajiri wake kusomesha vijana zaidi ya laki moja wa Afrika katika kipindi cha miaka 20.
“Ni
heshima kuu kupata nafasi ya kuthaminiwa na jarida lako, Ni heshima
kuwa miongoni mwa marafiki… tafadhali endelezeni kazi hii njema,”
alisema akizungumza kwa njia ya video.
Tuzo ya mfanyabiashara wa Mfano imeenda kwa Helen Hai, Mtendaji mkuu wa Made in Africa Initiative.
Tuzo hii kwa kawaida hutolewa kwa mtu aliyetoa mchango mkubwa katika kuboresha hali ya ufanyaji biashara barani Afrika.
Helen
ambaye ana asili ya China amewezesha mabadiliko makubwa katika biashara
ya viatu ya Ethiopia baada ya kuanzisha kiwanda cha viatu cha Huajian
Oktoba 2011 baada ya kuwa na mkutano na rais wa nchi hiyo Meles Zenawi
mwaka huo huo.
Imeelezwa
kuwa kiwanda hicho mara baada ya kuanzisha katika kipindi cha miezi
sita tu waliweza kuongeza pato la mauzo ya nje ya nchi hiyo kwa mara
mbili na katika kipindi cha miaka miwili kiliajiri waethiopia 4000.
Sasa hivi mdada huyo amefungua kiwanda cha nguo nchini Rwanda.
“Sekta
binafsi haikuja Afrika kutoa msaada, tumekuja afrika kufanyabiashara.
KLakini katika biashara tunatekeleza maelengo ya maendeleo. Nina imani
kubwa na Afrika, naamini kupitia simulizi za mafanikio tunashawishi
wengine kujiamini kutwaa uongozi na kuliwezesha bara hili kutambua fursa
zake,” alisema Helen.
Guaranty Trust Bank, iliwashinda wengine kadhaa waliotajwa na kushinda tuzo ya utawala bora wakati Abellon Clean Energy ilipata tuzio ya ubinifu wakati Nigerian Stock Exchange ilipata tuzo ya urejeshaji kwa jamii faida ikiwa ni huduma bora za jamii.
Akizungumzia
tuzo hizo ambazo ni za sab, Omar Ben Yedder alisema hafla hiyo
imwezeshwa na Zenith Bank, GTBank, Agility na Cofina .
Washindi wa 2015
AFRICAN BUSINESS OF THE YEAR
-Dangote, Nigeria
BUSINESS LEADER OF THE YEAR
-Mohammed Dewji, CEO, Mohammed Enterprise, Tanzania
MOST OUTSTANDING WOMAN IN BUSINESS
-Daphne Mashile Nkosi, Executive Chairperson, Kalagadi Manganese, South Africa
AWARD FOR GOOD CORPORATE GOVERNANCE
-Guaranty Trust Bank, Nigeria
AWARD FOR BEST CORPORATE SOCIAL RESPONSIBILITY
-The Nigerian Stock Exchange, Nigeria
AWARD FOR INNOVATION
-Abellon Clean Energy, Ghana
INSURANCE COMPANY & INITIATIVE OF THE YEAR
-BIMA ( bimamobile.com )
LIFETIME ACHIEVEMENT AWARD
-Strive Masiyiwa
AFRICAN BUSINESS ICON
-Helen Hai
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269