Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika ofisi za CCM Wilaya ya Kiteto kabla ya kuanzamikutano ya kampeni kunadi ilani ya CCM.
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wanachama wa CCM pamoja na wananchi wa Jimbo la Kilindi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni Mkoa wa Tanga. Miongoni mwa ahadi aliyoitoa kwa wanaKilindi ni kulishughulikia suala la upatikanaji wa huduma za maji safi na salama pamoja na ujenzi wa barabara ya kuingia na kutoka katika Wilaya hiyo.
Mgombea ubunge wa Jimbo la Kilindi, Mboni Muhita akionesha kwa wananchi nakala ya ilani ya uchaguzi ya chama hicho mara baada ya kukabidhiwa na mgombea mwenza kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni Mkoa wa Tanga.
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwenye mkutano wa hadhara Jimbo la Chemba.
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan akivishwa skafu kwa heshima na vijana wa UVCCM mara baada ya kuwasili katika Wilaya ya Kiteto ambapo alifanya mikutano ya kampeni kunadi ilani ya CCM.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM Taifa, Ummy Mwalimu (kushoto) na Mahadhi Juma wakijadili jambo kwenye moja ya mikutano ya kampeni ya mgombea mwenza.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269