Mtoto Loida Goodluck Kutoka shule ya Sekondari ya Simbani akichangia mada katika Mdahalo huo
Mjumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa mtoto Joyce Michael akizungumza jambo wakati wa Mdahalo huo
Jastin
Moses Mratibu wa mradi wa kuzuia ukatili dhidi ya mtoto kutoka Plan
International akichangia mchango wake wakati wa mdahalo huo
Ombeni Ally Mkuu wa Shule ya Sekondari Simbani akifafanua Jambo katika mdahalo huo
Ramadhan Lutambi mgombea udiwani kata ya Kibaha maili Moja kupitia Chadema akisisitiza Jambo
Rosemary Mkonyi mgombea Ubunge kupitia tiketi ya ACT akizungumza Jambo wakati wa mdahalo huo
Baadhi ya wanafunzi wakiwa wanasikiliza mdahalo huo
Wananchi wakiwa wanafuatilia kwa makini mdahalo huo
Na Mwandishi wetu
Jamii imetakiwa kuwa karibu zaidi na watoto ili kuhakikisha wanalindwa dhidi ya ukatili na kuhakikisha wanapata haki zao stahiki. Rai hiyo imetolewa na wakazi wa Kibaha Mkoani Pwani katika Mdahalo wa Walinde Watoto uliowaleta pamoja wapiga kura, watoto na wagombea wa nafasi za Ubunge na Udiwani.
Jamii imetakiwa kuwa karibu zaidi na watoto ili kuhakikisha wanalindwa dhidi ya ukatili na kuhakikisha wanapata haki zao stahiki. Rai hiyo imetolewa na wakazi wa Kibaha Mkoani Pwani katika Mdahalo wa Walinde Watoto uliowaleta pamoja wapiga kura, watoto na wagombea wa nafasi za Ubunge na Udiwani.
Kwa upande wake mgombea Ubunge
wa Kibaha vijijini kupitia ACT Wazalendo Dk. Rose Mkonyi alisema kuwa
chama chake kinaangalia ni kwa namna gani watazingatia katika Lishe bora
ya mtoto pamoja na namna gani mtoto atainuliwa Kielimu. Aidha Mgombea
Udiwani wa kata ya maili moja kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
‘CHADEMA’ Ramadhani Lutambi alisema chama chake kitaangalia zaidi afya
ya mtoto na kuhakikisha Bohari ya dawa inakuwa na dawa za kutosha.
Hata
hivyo, Watoto waliohudhuria mdahalo huo waliwataka wagombea kutimiza
ahadi wanazotoa wakati wa Kampeni ili na wao waweze kufikia malengo yao.
Watoto walipendekeza serikali ijayo iangalie namna ya kuwalinda hasa
wanapoelekea mashuleni kwani wamekuwa wakitembea mwendo mrefu kwenda na
kurudi shule ambako wamekuwa wakipata madhara na vishawishi vingi
wanapokuwa njiani.
Aidha watoto pia
waligusia suala la rushwa na kwa namna gani linavyorudisha nyuma
maendeleo yao na kuwaomba wagombea wa ngazi zote katika uchaguzi mkuu wa
mwaka huu kuwa waadilifu ili watoto wapate haki zao.
Mdahalo
huo ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production chini ya Wizara
ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto wakishirikiana na UNICEF uligusa
maeneo kumi muhimu ya uwekezaji kwa watoto ikiwemo kuwekeza kuokoa
maisha ya watoto na wanawake, kuwekeza kwenye lishe bora, kuwekeza
kwenye usafi, udhibiti wa miundombinu ya maji taka na ugavi wa maji
katika shule na kwenye huduma za afya pamoja na kuwekeza katika
kumwendeleza mtoto akiwa bado mdogo.
Mengine
ni pamoja na kuwekeza kwenye elimu bora kwa watoto wote, kuwekeza
katika kuzifanya shule kuwa mahali pa usalama, kuwekeza katika kuwalinda
watoto wachanga na wasichana dhidi ya VVU, kuwekeza katika kupunguza
mimba za utotoni, kuwekeza katika kuwanusuru watoto na vurugu,
udhalilishaji na unyonyaji pamoja na kuwekeza kwa watoto wenye ulemavu.
Vuguvugu
hili la kusambaza ajenda ya watoto kupitia midahalo na wagombea wa
nafasi mbalimbali linaendelea kupita mikoa mbalimbali nchini Tanzania
kwani tunaamini kuwekeza katika maeneo haya ya kipaumbele kunaweza
kupunguza umasikini na kuwezesha kuwepo kwa taifa linalostawi na la
usawa.
Unaweza
kusikiliza kipindi cha redio cha Walinde Watoto mahali popote kupitia
redio shiriki 19 ikiwemo TBC inayorusha matangazo hayo siku ya Jumamosi
kuanzia saa nane mchana na pia kupitia tovuti ya www.walindewatoto.org na
www.facebook.com/WalindeWatoto
www.facebook.com/WalindeWatoto
kawaida
Mtoto
Loida Goodluck Kutoka shule ya Sekondari ya Simbani akichangia mada
katika Mdahalo huo
Mjumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa mtoto Joyce Michael akizungumza
jambo wakati wa Mdahalo huo
Jastin Moses Mratibu wa mradi wa kuzuia ukatili dhidi ya mtoto kutoka
Plan International akichangia mchango wake wakati wa mdahalo huo
Ombeni Ally Mkuu wa Shule ya Sekondari Simbani akifafanua Jambo katika
mdahalo huo
Ramadhan Lutambi mgombea udiwani kata ya Kibaha maili Moja kupitia
Chadema akisisitiza Jambo
Rosemary Mkonyi mgombea Ubunge kupitia tiketi ya ACT akizungumza Jambo
wakati wa mdahalo huo
Baadhi ya wanafunzi wakiwa wanasikiliza mdahalo huo
Wananchi wakiwa wanafuatilia kwa makini mdahalo huo
Na Mwandishi wetu
Jamii imetakiwa kuwa karibu zaidi na watoto ili kuhakikisha wanalindwa
dhidi ya ukatili na kuhakikisha wanapata haki zao stahiki. Rai hiyo
imetolewa na wakazi wa Kibaha Mkoani Pwani katika Mdahalo wa Walinde
Watoto uliowaleta pamoja wapiga kura, watoto na wagombea wa nafasi za
Ubunge na Udiwani.
Kwa upande wake mgombea Ubunge wa Kibaha vijijini kupitia ACT Wazalendo
Dk. Rose Mkonyi alisema kuwa chama chake kinaangalia ni kwa namna gani
watazingatia katika Lishe bora ya mtoto pamoja na namna gani mtoto
atainuliwa Kielimu. Aidha Mgombea Udiwani wa kata ya maili moja kupitia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA’ Ramadhani Lutambi alisema
chama chake kitaangalia zaidi afya ya mtoto na kuhakikisha Bohari ya
dawa inakuwa na dawa za kutosha.
Hata hivyo, Watoto waliohudhuria mdahalo huo waliwataka wagombea
kutimiza ahadi wanazotoa wakati wa Kampeni ili na wao waweze kufikia
malengo yao. Watoto walipendekeza serikali ijayo iangalie namna ya
kuwalinda hasa wanapoelekea mashuleni kwani wamekuwa wakitembea mwendo
mrefu kwenda na kurudi shule ambako wamekuwa wakipata madhara na
vishawishi vingi wanapokuwa njiani.
Aidha watoto pia waligusia suala la rushwa na kwa namna gani
linavyorudisha nyuma maendeleo yao na kuwaomba wagombea wa ngazi zote
katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu kuwa waadilifu ili watoto wapate haki
zao.
Mdahalo huo ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production chini ya
Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto wakishirikiana na UNICEF
uligusa maeneo kumi muhimu ya uwekezaji kwa watoto ikiwemo kuwekeza
kuokoa maisha ya watoto na wanawake, kuwekeza kwenye lishe bora,
kuwekeza kwenye usafi, udhibiti wa miundombinu ya maji taka na ugavi wa
maji katika shule na kwenye huduma za afya pamoja na kuwekeza katika
kumwendeleza mtoto akiwa bado mdogo.
Mengine ni pamoja na kuwekeza kwenye elimu bora kwa watoto wote,
kuwekeza katika kuzifanya shule kuwa mahali pa usalama, kuwekeza katika
kuwalinda watoto wachanga na wasichana dhidi ya VVU, kuwekeza katika
kupunguza mimba za utotoni, kuwekeza katika kuwanusuru watoto na vurugu,
udhalilishaji na unyonyaji pamoja na kuwekeza kwa watoto wenye ulemavu.
Vuguvugu hili la kusambaza ajenda ya watoto kupitia midahalo na wagombea
wa nafasi mbalimbali linaendelea kupita mikoa mbalimbali nchini
Tanzania kwani tunaamini kuwekeza katika maeneo haya ya kipaumbele
kunaweza kupunguza umasikini na kuwezesha kuwepo kwa taifa linalostawi
na la usawa.
Unaweza kusikiliza kipindi cha redio cha Walinde Watoto mahali popote
kupitia redio shiriki 19 ikiwemo TBC inayorusha matangazo hayo siku ya
Jumamosi kuanzia saa nane mchana na pia kupitia tovuti ya
www.walindewatoto.org na
www.facebook.com/WalindeWatoto
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269