Mgombea wa urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia
wananchi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Sheikh
Amri Abeis jijini Arusha wakati akiwaomba wananchi wa jiji hilo
kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi wa
Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika nchini kote na kushirikisha
vyama mbalimbali vya kisiasa.
Amesema Mara atakapochaguliwa na
kuongoza taifa la Tanzania serikali yake itamuenzi Wazriri Mkuu wa
zamani kutoka jimbo la Monduli Mzee Edward Moringe Sokoine katika
kupambana na Rushwa ambapo mzee huyo hakupenda kabisa watu ambao ni wala
rushwa na wabadhirifu wa mali ya umma serikalini alipambana kufa na
kupona ili kuwasaidia wananchi waliowanyonge.
Katika mkutano huo pia wanachama
kadhaa waliokuwa viongozi wa Chama cha Demokrasia na Mendeleo CHADEMA
wamejiunga na chama cha Mapinduzi CCM na kutangaza rasmi katika mkutano
huo, wanachama hao ni Japhet Sironga aliyekuwa Mwenyekiti Chadema wilaya
ya Monduli na Jeremiah Mepukori Mwenyekiti BAVICHA wilaya ya Monduli
ambapo wamekabidhi kadi zao kwa Dk. John Pombe Magufuli na kadi hizo
kukabidhiwa kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.(PICHA NA
JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-ARUSHA)
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza
jambo wakati akihutubia katika mkutano huo wa kampeni uliofanyika jijini
Arusha leo.
Umati wa wananchi waliofurika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Arusha katika mkutano wa
kampeni wa mgombea wa CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Arusha katika mkutano wa
kampeni wa mgombea wa CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Mjumbe wa kamati ya ushindi ya CCM Ndugu Christopher Ole Sendeka akimnadi Dk. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.
Ni Full Nyomi tu Aursha.
Msanii Ali Kiba akitumbuiza katika mkutano huo.
Dk. John Pombe Magufuli na Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakiwa wamekaa meza kuu wakati
mkutano huo ukiendelea jijini Arusha kutoka kulia ni Ndugu Christopher
Ole Sendeka na Michael Lekule Laizer
Kindi la TOT likitumbuiza katika mkutano huo uliofanyika jijini Srusha.
Dk. John Pombe Magufuli na Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakicheza muziki mara baada ya
kuwasili kwenye mkutano katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini
Arusha.
Dk. John Pombe Magufuli na Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakimsikiliza mjumbe wa Kamati ya
Ushindi ya kampeni CCM Ndugu Christopher Ole Sendeka.
Baadhi ya akina mama wa kimasai wakiwa katika mkutano wa kampeni mjini Monduli.
Magufuli hapa kazi tu.
Dk. John Pombe Magufuli na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakiteta jambo walipkutana Longido.
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi
mgombea ubunge jimbo la Monduli Namelok Sokoine kwenye mkutano wa
kampeni uliofanyika Mtowambu wilayani Monduli.
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwanadi
baadhi ya wagombea ubunge mkoa wa kulia ni Philemon Molel mgombea ubunge
jimbo la Arusha mjini na kutoka kulia ni Catherine Magige na Viola
Mfuko wagombea ubunge viti maalum CCM mkoa wa Arusha.
Namelok Sokoine Mgombea Ubunge
jimbo la Monduli akiomba kura kwa wananchi wa Monduli ili awe mbunge wa
jimbo hilo na kuanzisha historia mpya kwa kuwa mbunge wa kwanza mwanamke
wa jimbo hilo.
Jeremiah Mepukori aliyekuwa
Mwenyekiti BAVICHA wilaya ya Monduli akikabidhi kadi yake kwa Dk. John
Pombe Magufuli huku Japhet Sironga aliyekuwa Mwenyekiti Chadema wilaya
ya Monduli mwenye kofia akifurahia baada ya wote kujiunga na CCM jijini
Arusha leo.
Arusha ni Magufuli tu leo.
Wasanii mbalimbali wakiimba wimbo maalum kwa ajili ya kampeni za Dk. John Pombe Magufuli uliozinduliwa leo jijini Arusha.
Wasanii wakiimba wimbo huo.
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwana
viongozi mbalimbali wakiwa katika jukwaa kuu kwenye mkutano huo jijini
Arusha.
Yamoto Band wakafanya mambo makubwa sana Sheikh Amri Abeid.
Wabunge wanaogombea ubunge viti
maalum mkoa wa Arusha CCM Viola Mfuko na Catherine Magige wakiwatunza
vijana wa Yamoto Band wakati walipokuwa wakitumbuiza kwenye mkutano wa
kampeni wa CCM jijini Arusha.
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga
wananchi wa jiji la Arusha mara baada ya kuwahutubia kwenye mkutano
uliofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269