Breaking News

Your Ad Spot

Oct 11, 2015

MAJIMAJI SEREBUKA MARATHON YAUNGURUMA SONGEA


Wakali wa marathon wakitayarisha saa zao, tayari kwa kuanza safari ya Km 42, katika tamasha la kila mwaka la Majimaji Selebuka 2015 linaloendelea kwenye Uwanja wa Makumbusho ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji, Songea.

Washiriki wa mbio ndefu za Km 42 katika Tamasha la Majimaji Selebuka 2015, wakichanja mbuga. Kutoka kushoto ni Paulo Modest, Isaki Naghali na Shauri Gwaangwi. Tamasha hilo linaendelea katika Uwanja wa Makumbusho ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji, Songea.

Bingwa wa mbio za Km 21 za mashindano ya Tamasha la Majimaji Selebuka 2015, Mohamed Dule akimalizia mbio. Tamasha hilo linaendelea kwenye 2015 linalofanyika kwenye Uwanja wa Makumbusho ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji, mjini Songea.(P.T)
Mwanariadha wa mbio za Km 21, Sanslaus Tseama.Shauri Gwaangwi, mshiriki wa mbio ndefu za Km 42 katika Tamasha la Majimaji Selebuka akipata huduma ya maji.
Washindi wa mbio fupi za kilometa tano kwa upande wa wanawake, Neema Ndambo wa pili kulia na Faraja Ndambo wakiwa na viongozi wa tamasha hilo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Asasi ya Somi, Julian Murchison na Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Ruvuma, Christian Matembo.
Washindi wa mbio mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Tamasha la Majimaji Selebuka 2015.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages