Aliyekuwa
Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji akisalimiana na mmoja
wa madiwani waliofika kumpokea mara tu baada ya kuwasili katika uwanja
wa ndege wa Singida mjini pamoja na wasaidizi wake.(Picha zote na Zainul
Mzige wa Modewjiblog).
Aliyekuwa
Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji akiwa ameambatana na
Mgombea Ubunge wa jimbo la Bumbuli, January Makamba ambaye pia ni mmoja
wa wanakamati wa timu ya ushindi ya kampeni za Mgombea urais kupitia
tiketi ya CCM, Dk.John Pombe Magufuli, wakielekea sehemu ya mapokezi
mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege Singida mjini.
Aliyekuwa
Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji akilakiwa kwa furaha
na watoto wanaoishi kwenye eneo la uwanja wa ndege Singida mjini.
Watoto
wakimpokea kwa shangwe aliyekuwa Mbunge wao jimbo la Singida mjini,
Mohammed Dewji mara tu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege Singida
mjini kwa ajili ya kuhudhuria kampeni za Mgombea urais kupitia tiketi ya
CCM, Dk.John Pombe Magufuli pamoja na kumuombea kura kwa wana Singida.
Pichani juu na chini ni Mohammed Dewji akibadilishana mawazo na watoto waliojitokeza kumpokea uwanjani hapo.
Aliyekuwa
Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji akiagana na Mgombea
Ubunge wa jimbo la Bumbuli ambaye pia ni mmoja wa wanakamati wa timu ya
ushindi ya kampeni za Dkt. Magufuli, January Makamba kabla ya kuelekea
kwenye viwanja vya Peoples Singida mjini ulipofanyika mkutano wa kampeni
za Mgombea urais kupitia tiketi ya CCM, Dk.John Pombe Magufuli. Kulia
ni Msaidizi wa MO, Duda Jumanne.
Aliyekuwa
Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji akipata picha ya
ukumbusho na wanaSingida wanaoishi karibu na maeneo ya uwanja wa ndege
wa Singida mjini.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269