Mwanahabari
na blogger wa mtandao wa modewjiblog.com, Andrew Chale akiwa katika
geti kuu la kuingilia katika ofisi za Hifadhi ya Taifa ya Udzungwa
zilizopo eneo la Mang'ula, Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro,
Tanzania. Alipokuwa katika habari za Utafiti jinsi ya Mabadiliko ya
Tabianchi yanavyoathiri mbuga na hifadhi za Taifa nchini (How Climate
Change Effect The National Parks in Tanznia) hivi karibuni (Picha na
modewjiblog).
TABIANCHI YAWEKA HIFADHI ZA TANZANIA HATARINI
Na Andrew Chale, modewjiblog
[TANZANIA]
Zimebaki siku zaidi ya 60, kuelekea mkutano mkuu wa 21 (COP21) wa nchi
wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Nchi (UNFCCC) unaotarajiwa
kufanyika Paris, Ufaransa. mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka huu.
Dulu
na chunguzi za kitafiti zinaeleza kuwa, Tanzania ni miongoni mwa
Mataifa Barani Afrika yatakayokumbwa na janga kubwa dhidi ya Mabadiliko
ya tabianchi (Climate Change in Tanzania National Parks) kwenye
Hifadhi na mbuga zake.
Dulu
hizo za kitafiti pia zinabainisha kuwa, asilimia kadhaa za Wanyama nao
watatoweka kabisa hali ambayo taifa litakumbwa na matatizo mbalimbali
ikiwemo kushuka kwa uchumi wa Nchi katika siku za usoni.
Hivi
karibuni, mwandishi wa Makala haya wa modewjiblog, alipata kutembelea
Hifadhi kadhaa za taifa zilizo chini ya usimamizi wa Shirika la Hifadhi
la Taifa, Tanzania National Parks Authority (TANAPA). Hifadhi hizo
zikiwepo Udzungwa, Selous Game Reserve, Mikumi, Ruha, na Saadan
pamoja na kuonana na wataalamu wa mabadiliko ya tabianchi kwenye idara
za serikali na watu binafsi.
Eneo la kuingia katika Hifadhi na makao makuu ya hifadhi ya Udzungwa...
Hifadhi ya Taifa ya Udzungwa:
Kwa
mujibu wa tovuti ya Serikali inabainisha kuwa Udzungwa ni miongoni mwa
milima yenye Bionuwai nyingi iliyozungukwa na misitu.
Hata
hivyo vyanzo mbalimbali vinabainisha kuwa, Hifadhi hii ya Udzungwa ni
miongoni mwa Hifaadhi zilizo kwenye hatari ya kutoweka kutokana na
mipango hafifu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Vyanzo
vya ndani vinaeleza kuwa, ili kukabiliana na hali ya mabadiliko ya
tabianchi yasiathiri Hifadhi hizo, juhudi za haraka zinahitajika
kuchukuliwa ikiwemo wasimamizi na wananchi wanaozunguka hifadhi kupewa
elimu ya kutosha pamoja na mipango kazi ya mara kwa mara.
Bwana
Ruombano Mnege (56) mkazi wa kijiji cha Msolwa katika eneo jirani na
hifadhi ya Udzungwa anaeleza kuwa, afahamu maana ya mabadiliko ya
tabianchi, ila anachoelewa ni kuwa mambo yanabadilika pindi Mungu
anapoamua.
"Mimi
natambua Mungu anapoamua ndio mambo yanatokea. Suala la mabadiliko ya
tabianchi kwa sie wa huku hasa wakulima hatutambui sana kwa sababu
hatuna elimu ya kutosha” alibainisha Mnege akijibu maswali endapo
wasimamizi wa hifadhi hizo kama wanawashirikisha wananchi katika
kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Hata
hivyo, wakazi wengi wa maeneo ya jirani na hifadhi wanabainisha kuwa,
hawana elimu ya kutosha katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi,
hali inayowapa hofu kukumbwa na janga hilo la ukame siku za usoni.
Ambapo
walibainisha kuwa, wapo watu wasio waaminifu wakiingia katika hifadhi
hizo na kukata miti pamoja na kuharibu vyanzo vya maji, kuchoma moto
misitu pamoja na kuwinda wanyama.
"Kulikuwa
na wanyama wakifika hadi kwenye mashamba yetu miaka ya nyuma. Lakini
kwa sasa wanyama wale hawafiki kabisa kutokana na hali ilivyo huenda
wamepotea” anaeleza Bi. Jonesia Simon mkazi wa Sanje ambapo anasema
kutoonekana kwa wanyama hao kwa hivi sasa kumechangiwa na mabadiliko ya
tabianchi kwani kulikuwa na wanyama waliokuwa wakifuata maji na
wengine walikuwa wakifuata vyakula kwenye mashamba hayo lakini kwa sasa
wametoweka kabisa.
Mwandishi
wa makala haya, Andrew Chale wa modewjiblog.com akiwa katika eneo la
Sanje wakati wa kupanda mlima Udzungwa kuelekea kwenye maporoko ya
Udzungwa (Picha na modewjiblog team).
ramani inayoonyesha hifadhi hiyo ya Udzungwa..
Milima
ya udzungwa ni jina la hifadhi inayopatikana hifadhi hiyo ndani ya
Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro pamoja na upande wa Iringa. Milima
hii ni makazi ya wanyama pori wa aina mbalimbali huku ikiwa na ukubwa
wa kilometa 1990.
Udzungwa
ni miongoni mwa hifadhi zenye hazina ya aina nyingi za mimea, ndege na
wanyama ambao hawapatikani katika sehemu nyingine duniani.
Hifadhi
iko umbali wa kilometa 350 kusini mwa Dar es Salaam, kilometa 65 kutoka
katika Hifadhi ya Mikumi ambayo ni ya jirani kabisa.
Kati
ya aina sita za jamii ya nyani wanaopatikana katika hifadhi hii, mbili
hupatikana katika hifadhi hii pekee ambao ni : Mbega Mwekundu, wa Iringa
(Iringa red colobus monkey) na aina ya pili ni Sanje Crested mangabey.
Huku
kukiwa na aina mbalimbali za ndege na aina nne za ndege ambao
hazikufahamika hadi katika miaka ya karibuni. Ndege ni Chozi bawa
jekundu (rufous-winged sunbrid) na wengine wengi akiwemo kwale
Udzungwa.
Hifadhi hii pia ni moja ya makazi makuu na muhimu ya ndege pori barani Afrika.
Picha
ya juu Maporoko hayo na chini ni Mwandishi wa makala haya wa
modewjiblog.com, Andrew Chale akiwa kwenye maporomoko hayo ya Udzungwa
wakati alipotembelea kuandika habari za Mabadiliko ya Tabianchi namna
yanavyoweza kuathiri Hifadhi za Taifa nchini. (Picha na modewjiblog
team).
Mwandishi
wa makala haya wa modewjiblog.com, Andrew Chale akiwa katika eneo la
awali na mapumziko baada ya safari ndefu ya kupanda mlima huo katika
kuelekea kwenye maporomoko hayo ya Udzungwa (Picha na modewjiblog team).
Maporomoko ya Sanje:
Ndani
ya hifadhi hii pia ina Mto Sanje ambao ni kivutio kikubwa sana. Mto
huu una maporomoko ya maji yenye urefu wa mita zipatazo 170 yakianguka
kupitia msituni na kututa mithili ya mianzo ya ukungu bondeni.
Hata
hivyo, mbali na kuwa na vitu vyote hivyo ndani ya hifadhi hii ya
Udzungwa, Serikali na jamii inayozunguka hiafdhi hii inawajibu mpana wa
kukabiriana na mabadiliko ya tabianchi kwani wasipochukua hatua vitu
hivyo vinaweza kutoweka na nchi ikaja kukosa mapato kwani Utalii ni
miongoni mwa sekta inayoiingizia Tanzania fedha nyingi za kimaendeleo.
Wanyama kutoweka:
Tovuti ya Serikali ya Makamu wa Rais (http://www.vpo.go.tz/news),
imebainisha kuwa: Inakadiriwa kwamba asilimia 34 ya ardhi ya Bara la
Afrika iko katika hatari ya kugeuka jangwa kutokana na mabadiliko ya
TabiaNchi.
Na
kuongeza kuwa: Hali hii ya mabadiliko ya TabiaNchi itachangia kutoweka
kwa asilimia kati ya 25 hadi 40 ya aina fulani za wanyama katika
hifadhi Barani Afrika ifikapo mwaka 2020 na kwamba maeneo kame
yataongezeka kwa asilimia 5 hadi 8 Barani Afrika ifikapo mwaka 2080.
Msemaji wa TANAPA:
Hata
hivyo suala la mabadiliko ya tabianchi katika hifadhi za Taifa nchini
bado halijapewa kipaumbele kikubwa hasa kwa wadau wa mabadiliko ya
tabianchi ikiwemo wanahabari, wanaharakati wa mazingira na wananchi
wanaoishi jirani na hifadhi. Hii inatokana na hata wakati mwingine
kukosa ushirikiano wa karibu kutoka kwa mamlaka husika ikiwemo makao
makuu ya ofisi za TANAPA ambao ndio wenye jukumu la kutoa taarifa za
kina kitaalamu.
Mwandishi wa makala haya akiwa katika view point ya maporomoko hayo..
Taswira
ya eneo la maporomoko ya Udzungwa inavyoonekana unapokuwa katika eneo
la awali la View Point ndani ya Hifadhi hiyo ya Udzungwa. Katika taswira
hiyo panaonekana kama ramani ya Afrika. (Picha na Andrew
Chale,modewjiblog).
eneo
la maji yanayotoka kwenye maporomoko hayo ambapo kwa kipindi hiki
yanapoonekana yakiwa yamepungua kutokana na kipindi maalum. Hata hivyo
maji hayo kuna msimu yanajaa zaidi ..
Miongoni
mwa aina za ndege wanaopatikana ndani ya hifadhi hizo za Udzungwa
ambapo inaelezwa kuwa Hifadhi hiyo imekuwa ikitembelewa na ndege
mbalimbali kutoka maeneo mengi ya nchi za Afrika.
Miongoni mwa miti inayopatikana ndani ya misitu hiyo ya Hifadhi ya Udzungwa..
Miongoni
mwa miti inayopatikana ndani ya Hifadhi hiyo ambayo hata hivyo bado
inakabiriwa na changamoto kwa watu wasio na mapenzi mema kuvamia na
kukata miti hiyo ya hifadhi kwa ajili ya shughuli za mbao na mambo
mengine.
Miongoni
mwa miti ambayo inapatikana ndani ya hifadhi hiyo ambayo ni dawa na pia
ni miongoni mwa miti inayopendwa na wanyama hata hivyo ipo katika
changamoto ya kutoweka...
Red Col wanaopatikana ndani ya Misiti hiyo ya Hifadhi ya Udzungwa..
Mwandishi
wa makala haya wa modewjiblo, Andrew Chale akiwa katikati ya Hifadhi
hiyo wakati wa kuyatafuta Maporomoko hayo. Ambapo ndani ya msitu huo
wenye baridi muda wote kutokana na kuzungukwa na miti mbalimbali.
Misitu hiyo ya Udzungwa inavyoonekana..
Itaendelea ripoti sehemu ya Pili…
Ripoti hii imeandaliwa na Andrew Chale, Mwandishi wa Habari na Mhariri wa mtandao (blog) ya modewjiblog.com ya nchini Tanzania. ( Anuani : +255719076376 au barua pepe: andrewchale@gmail.com).
Makala
haya yamefadhiliwa na kwa ufadhili wa Shirika la ( CFI) la nchini
Ufaransa, chini ya mradi wa Medias 21 Africa & Asia.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269