Naibu Waziri Wizara ya Nishati na
Madini Dkt. Medadi Kalemani (wa kwanza kulia) akitoa maagizo ya
kukamilika kwa mradi huo ifikapo february mwakani kwa Mkurugenzi
Mwandamizi wa Miradi TANESCO Bw.Gregory Chegere (wa kwanza kushoto)
alipofanya ziara yake leo katika mradi wa Tanzania Energy Development
Access Program (TEDAP) eneo la Mbagala Rangi Tatu,jijini Dar es
Salaam,Mradi huo utasaidia kusambaza umeme wenye nguvu ya kutosha na
unaotarajia kunufaisha zaidi ya wananchi elfu kumi wa eneo hilo,watatu
kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Paul
Masanja.
Naibu Waziri Wizara ya Nishati na
Madini Dkt. Medadi Kalemani (kushoto) akitoa maagizo kwa Mkandarasi wa
Kampuni ya SAE Power Lines Bw.Tahir Mehmood (wa kulia) anayejenga mradi
wa TEDAP eneo la Kurasini jijini Dar es salaam kuhakikisha mpaka
mwanzoni mwa mwakani awe amshafunga Transifoma katika eneo hilo la mradi
ni baada ya kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wake katika mradi
huo.
Mhandisi Mkuu wa Miradi TANESCO
Bw. Frank Mashalo (wa kwanza kulia) akimweleza Naibu Waziri Wizara ya
Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani (wa pili kushoto)kuhusu maendeleo
ya mradi TEDAP uliyopo maeneo ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam
na (wa kwanza kushoto) ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini
Mhandisi Paul Masanja.
Naibu Waziri Wizara ya Nishati na
Madini Dkt. Medadi Kalemani (kushoto) akisikiliza malalamiko ya mmoja
wa wateja wa huduma za TANESCO Bw.Michael Sedyan, Mkazi wa Sinza,hii ni
baada ya Naibu waziri kufanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za
Tanesco Magomeni leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Muendesha Mitambo kituo cha
TANESCO Kipawa Bibi Zuhura Mmanyi (wa kwanza kulia)akimweleza Naibu
Waziri Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani (wa kwanza
kushoto) namna mitambo ya eneo hilo inavyofanya kazi na maeneo mitambo
hiyo inayosambaza umeme ikiwemo eneo la Gongo la
mboto,Kiwalani,Segerea,Chang’ombe na Buguruni leo jijiji Dar es Salaam
Naibu waziri alipo fanya ziara yake katika ofisi hiyo (wapili kushoto ni
Mkurugenzi Mwandamizi wa Miradi TANESCO Bw.Gregory Chegere na wapili
kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Paul
Masanja.
Naibu Waziri Wizara ya Nishati na
Madini Dkt. Medadi Kalemani (wa kwanza kushoto) akitoa maagizo kwa
Mkandarasi wa Kampuni ya SAE Power Lines Bw.Stephen Joseph (wa kwanza
kulia) anayejenga Mradi wa TEDAP eneo la Gongo la Mboto kuhakikisha
umeme unaanza kuwaka katika mitambo hiyo ifikapo mwishoni mwa mwezi
Desemba 2015 kwa kuwa kila kitu kimeshakamilika katika mradi huo na
malipo yake tayari ameshamaliziwa kulipwa, (wapili kushoto) ni
Mkurugenzi Mwandamizi wa Miradi TANESCO Bw.Gregory Chegere.
Naibu Waziri Wizara ya Nishati na
Madini Dkt. Medadi Kalemani (kulia) akimsikiliza mmoja wa wateja wa
Ofisi ya TANESCO Magomeni Bw.Mohamed Bago Mkazi wa Manzese alipokuwa
akitoa kero yake kuhusu kusubiri zaidi ya masaa matatu kupatiwa huduma
ya tatizo ya luku yake ambayo haiingizi umeme,hiyo ni baada ya kufanya
ziara ya kushtukiza katika ofisi za Tanesco Magomeni.
Picha na Na Anitha Jonas –MAELEZO
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269