WAZIRI Mkuu wa zamani wa Israeli, Bw. Ehud Olmert, akiwa mahakami mjini Jerusalem
Na K-Vis Media na Mashirika ya Habari
WAZIRI
Mkuu wa zamani wa Israeli, Bw. Ehud Olmert, ametupwa jela baada ya kupatikana
na hatia ya kula “mlungula” RUSHWA.
Olmert
ambaye amerithiwa na Waziri Mkuu wa sasa Benjamin Netanyahu, alihukumiwa
kifungo cha miaka 6 jela na mahakama ya chini mnamo mwaka 2014, lakini adhabu
hiyo ilipunguzwa na mahakama kuu hadi kufikia kifungo cha miezi 18 jela leo
Jumatatu Desemba 28, 2015.
Olmert
mwenye umri wa miaka 70, aliendesha operesheni ya kuwashambulia Hezbollah huko
Lebanon, wakati wa utawala wake na kusababisha vifo vingi, alihukumiwa kufuatia
mikataba ya majumba ya kupangisha wakati huo akiwa Meya wa mji wa Jerusalem
kabla ya kuwa waziri Mkuu mnamo mwaka 2006.
Olmert
ambaye aliondoka madarakani mnamo mwaka 2009, anakuwa Kiongozi wa juu wa kwanza
wa Israeli kutupwa jela na anatarajiwa kuanza kutumikia kifungo chake mnamo
Februari 15 mwaka ujao 2016
Akijadiliana jambo na wakili wake
Akiwa mahakamani
Wakati huo akiwa madarakani
Akiwasili mahakamani huku akisindikizwa na walinzi wake |
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269