Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua dagaa wanaokaushwa kitalaam kwa kutumia jua wakati alipozindua soko na mwaro wa kisasa wa samaki wa Kibirizi mjini Kigoma Desemba 28, 2015.
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizindua soko na Mwaro wa samaki wa Kibirizi mjini Kigoma Desemba 28 , 2015.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo Issa Machibya.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Kigoma, Issa Machibya kuhusu bunduki iliyokatwa ili kupunguzwa urefu ambayo ilikamatwa na polisi mkoani Kigoma wakati ilipotumika katika uhalifu. Majaliwa alikwenda kwenye Ofisi ya Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kigoma kuona silaha mbalimbali zilizokamatwa na polisi Desemba 28, 2015.
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akitazama kifaa kinachotumiwa na wahalifu kutengeneza risasi za bunduki aina ya goboli wakati alipokagua silaha mbalimbali zilizokamatwa na polisi mkoani Kigoma na kuhifadhiwa kwenye Ofisi ya Kamanda wa polisi wa mkoa huo, Desemba 28, 2015.
Mkazi wa Kigoma mjini akionyesha bango katika mkutano uliohutubiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye soko la samaki la Kibirizi mjini Kigoma Desemba 28, 2015.
Watumishi wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majliwa wakati alipowahutubia mjini Kigoma Desemba 28, 2015.
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na watumishi wa serikari Kuu na Serikali za Mitaa mjini Kigoma Desema 28, 2015. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Your Ad Spot
Dec 29, 2015
Home
Unlabelled
ZIARA YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA MKOANI KIGOMA
ZIARA YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA MKOANI KIGOMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269