Amiri
Jeshi Mkuu Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Luteni Jenerali
Venance Salvatory Mabeyo kuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Ikulu jijini Dar
es salaam leo January 30, 2016. Awali Luteni Jenerali Mabeyo alikuwa
Mkuu wa Idara ya Usalama na Utambuzi Jeshini na anachukua nafasi ya
Luteni Jenerali Samwel Ndomba. Rais pia amewaapisha Kamishna wa Polisi
wa Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja kuwa Katibu Tawala mkoa wa
Katavi, huku aliyekuwa Mkuu wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Polisi,
Kamishna Clodwin Mtweve kuwa Katibi Tawala mkoa wa Mwanza. Naye
Dkt.Mahafhi Juma Maalim aliapishwa kuwa balozi mpya wa Tanzania nchini
Kuwait (Habari na K-VIS MEDIA/Khalfan Said, Picha na Ikulu).
Rais akimpongeza Luteni Jenerali Mabeyo kwa wadhifa huo mpya.
Rais katika picha ya pamoja na Mnadhimu Mkuu mpya wa Jeshi, Luteni Jenerali Mabeyo, na mtangulizi wake, Luteni Jenerali Ndomba.
Rais katika picha ya pamoja na Mkuu wa
Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange(wapili kushoto), Mkuu WA Jeshi la
Polisi, IGP, Ernest Mangu(watatu kulia), Mnadhimu Mkuu mpya wa Jwtz,
Luteni Jenerali Mabeyo,(wapili kulia), katibu Tawala mkoa wa Katavi,
Kamishna Paul Chagonja,(wakwanza kulia) na katinu Tawala mkoa wa Mwanza,
Kamishna Vlodwin Mtweve (wakwanza kushoto), Mara baada ya hafla ya
viapo.
Rais akimkabidhi vitendea kazi Kamishna Chagonja baada ya kumuapisha
Rais akimuapisha balozi Mahadhi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269