Kikao cha kupiga kura ya kuwa na imani na serikali mpya ya umoja wa
kitaifa ya Libya katika Bunge la Taifa la nchi hiyo linalotambuliwa
rasmi na jamii ya kimataifa, kimeahirishwa tena.
Awali ilipangwa kuwa kikao hicho kingefanyika jana lakini
kimeahirishwa. Mbunge Aisha al Aqouri wa Libya amesema kuwa wawakilishi
wenzake 118 waliokuwepo bungeni hiyo jana walichukua uamuzi wa wa kumpa
Waziri Mkuu wa Libya fursa ya hadi kufikia Jumanne ijayo kwa ajili ya
kuarifisha mawaziri wa serikali yake.
Serikali mpya ya Libya ilitangazwa Jumapili iliyopita chini ya
usimamizi wa Umoja wa Mataifa. Serikali hiyo ina mawaziri 13 na mawaziri
washauri 5.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269