Mwanasiasa wa Misri Boutros Boutros-Ghali aliyekuwa Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa kuanzia mwaka 1992 hadi 1996 amefariki dunia.
Boutros Boutros-Ghali alifariki dunia jana akiwa na umri wa miaka 94.
Rafael Ramires, mwanadiplomasia wa Venezuela ambaye ndiye rais wa
sasa wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa alitangaza jana habari hiyo
katika kikao cha baraza hilo kilichokuwa kikijadili suala la Yemen na
kutaka hadhirina wanyamaze kimya dakika moja kwa mnasaba wa kufariki
dunia mwanasiasa huyo mkongwe wa Misri.
Katika kipindi cha uongozi wake kwenye Umoja wa Mataifa, Boutros
Boutros-Ghali alichukua hatua za kufanyia marekebisho muundo wa
sekretarieti ya umoja huo na kupanua zaidi maana ya operesheni za mapema
kwa ajili ya kulinda amani duniani.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269