Mwakilishi wa kudumu wa Syria katika Umoja wa Mataifa amesema
matatizo na mashaka ya sasa ya dunia ni matunda ya siasa za Magharibi
hususan Marekani.
Bashar Ja'fari ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
kwamba, wawakilishi wa Marekani, Uingereza na Ufaransa wamesahau maafa
yaliyosababishwa na siasa za nchi zao katika nchi za Mashariki ya Kati
kwa miongo kadhaa iliyopita. Amesema tangu mwanzoni nchi hizo zilianza
kutekeleza siasa za kuiunga mkono Israel na kuitayarishia uwanja wa
kuzikalia kwa mabavu ardhi za nchi za Kiarabu na zimetumia makumi ya
kura ya veto kuukingia kifua utawala huo ghasibu ili watu wa Mashariki
ya Kati waendelea kuishi katika mashaka na tabu.
Kuhusu suala la mapambano dhidi ya ugaidi, mwakilishi wa kudunu wa
Syria katika Umoja wa Mataifa amesema, njia pekee ya kuaminika katika
uwanja huo ni kuunda muungano wa kimataifa kwa mujibu wa sheria za
kimataifa na kwa kuzishirikisha nchi zote husika hususan Syria.
Amezilaumu baadhi ya nchi kuwa zimekiuka hati ya Umoja wa Mataifa kwa
kutuma majeshi katika ardhi ya Syria bila ya idhini ya nchi hiyo na
kuficha harakati za magaidi kwa kutumia kisingizio cha kupambana na
ugaidi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269