Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, eneo la kusini mwa Afrika
linakabiliwa na ukame wa hali ya juu unaotishia maisha ya mamilioni ya
watu.
Taarifa iliyotolewa jana Jumanne na umoja huo imesema kuwa,
karibu watu milioni 49 wa eneo la kusini mwa Afrika, wanakabiliwa na
hali ya ukame wa kutisha ambao umeshadidishwa na athari za El Nino.
Umoja wa Mataifa umesema, watu milioni 14 katika eneo hilo ndio
wanakabiliwa na hali mbaya zaidi na umesisitiza kuwa, kupungua kwa mvua
katika misimu ya masika baina ya Oktoba hadi Disemba kuanzia mwaka 1981
hadi leo na kuibuka kwa janga la El Nino kumesababisha hali mbaya katika
maeneo hayo ya kusini mwa Afrika.
Kabla ya hapo Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO)
lilikuwa limetangaza kuwa, utabiri unaonyesha kuwepo uwezekano wa
kuendelea kwa uhaba wa mvua kati ya Januari na mwezi Machi. Kupungua kwa
mvua na kupanda kwa bei za vyakula katika eneo hilo hususan nchini
Malawi, kumeifanya hali kuwa mbaya zaidi na kuhatarisha maisha ya karibu
watu milioni tatu wa nchi hiyo.
Mbali na Zambia, watu milioni mbili nchini Madagascar na karibu watu
milioni moja na nusu huko Zimbabwe wanakabiliwa na njaa kali inazotokana
na taathira hizo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269