Afisa wa zamani wa jeshi la Marekani amesema kuwa silaha za kemikali zinazomilikiwa na kundi la Daesh zimetoka Marekani.
Katika mahojiano yake ya IRIB, Scott Bennett ambaye aliwahji kuwa
afisa wa jeshi la Marekani amelaani jinai zinazoendelea kufanywa na
wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh katika nchi za Iraq na Syria na
kusema, kundi hilo linamiliki silaha za kemikali kutoka Marekani na
kwamba lilipata silaha hizo hatari kupitia Saudi Arabia na Uturuki.
Bennett amesema kuwa Serikali na Congresi ya Marekani zimelipa kundi
hilo la kigaidi silaha hizo za kemikali kwa makusudi ili litimize
malengo ya Washington katika eneo la Mashariki ya Kati. Afisa huyo wa
zamani wa jeshi la Marekani ameongeza kuwa, Washington imeshindwa
kufikia malengo yake nchini Syria kwani licha ya miaka kadhaa ya ngogoro
wa ndani nchini humo Wasyria bado wana imani na serikali ya Rais Bashar
Assad na wanashiriki katika medani za vita dhidi ya kundi la Daesh kwa
lengo la kurejesha amani na utulivu katika nchi yao.
Mgogoro wa ndani wa Syria ulianza mwaka 2011 kufuatia hujuma na
mashambulizi makubwa ya makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na Marekani
na waitifaki wake wakubwa kama Saudi Arabia kwa shabaha ya kuiondoa
madarakani serikali halali ya Rais Bashar Assad.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269