Kamishna
Jenerali John Casmir Minja akipokea Salaam ya Utii kutoka kwa Gadi
Maalam iliyoandaliwa na Maofisa wa Jeshi la Magereza, Wahitimu wa
Mafunzo ya Udereva (hawapo pichani) katika Chuo cha Udereva Kingolwira
Mkoani Morogoro. Hafla hiyo imefanyika katika Viwanja vya Chuo hicho 16
Februari, 2016.
Kamishna
Jenerali wa Magereza John Casmir Minja akikagua Gadi Maalum
iliyoandaliwa na Wahitimu wa Mafunzo ya Udereva katika Chuo cha Udereva
na Ufundi Kingolwira, Mkoani Morogoro.
Wahitimu wa Mafunzo hayo wakipita mbele ya Mgeni rasmi katika mwendo wa kasi kama wanavyoonekana katika picha.
Kamishna
Jenerali wa Magereza John Casmir Minja akipokea taarifa fupi Ofsini kwa
Mkuu wa Chuo cha Udereva na Ufundi Kingolwira, Kamishna Msaidizi wa
Magereza, Osmond Nduguru (hayupo pichani).
Kamishna
Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja akimtunuku cheti Askari Mhitimu
wa Mafunzo ya Udereva kwa niaba ya Wahitimu wote wa mafunzo hayo.
Baadhi
ya Waandishi wa Habari wa Mkoani Morogoro wakifanya Mahojiano Maalum na
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja.
Mgeni
rasmi, Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja (katikati) akiwa
katika picha ya pamoja na Wahitimu wa Mafunzo ya Udereva katika Chuo cha
Udereva na Ufundi, Kingolwira Mkoani Morogoro.
…………………………………………………………………………………………….
…………………………………………………………………………………………….
Na Lucas Mboje; Morogoro
MADEREVA
wote wa magari ya Jeshi la Magereza nchini wametakiwa kuzingatia Sheria
za Usalama Barabarani wakati wote wanapoendesha magari ili kujiepusha
na ajali zisizo za lazima.
Rai
hiyo imetolewa na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir
Minja wakati akizungumza kwenye hafla ya kufunga Mafunzo ya Udereva Kozi
ya Msasa kwa Maofisa wa Jeshi la Magereza kutoka Mikoa yote Tanzania
Bara yaliyofanyika katika Chuo cha Udereva na Ufundi, Kingolwira Mkoani
Morogoro.
Jenerali
Minja amewaagiza Wahitimu wa Mafunzo hayo kuhakikisha kuwa wanawajibika
pia kuyatunza magari watakayokabidhiwa kuyaendesha ili yaweze kudumu
kwa muda mrefu kama ilivyokusudiwa.
“Nawataka
mjiepushe na uzembe wakati mnapoendesha magari ya Jeshi letu ikiwa ni
pamoja na kutokujihusisha na ulevi na kuendesha magari hayo kwa mwendo
kasi bila kuzingatia Sheria za Usalama Barabarani”. Alisema Jenerali
Minja.
Aidha
Jenerali Minja amezungumzia upungufu mkubwa wa magari katika Jeshi
hilo ambapo katika kushughulikia changamoto hiyo Jeshi la Magereza
kupitia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa limesaini Mkataba na
Kampuni za Ashok Layland na Jeep na magari mia tisa na tano(905)
yanategemewa kupokelewa mapema mwanzoni mwa mwezi Mei Mwaka huu.
Kwa
upande wake Mkuu wa Chuo cha Udereva na Ufundi Kingolwira, Kamishna
Msaidizi wa Magereza, Osmond Ndunguru kupitia risala yake kwa Mgeni
rasmi amesema kuwa Wahitimu hao wamejifunza Mafunzo yote yaliyopo kwenye
Mtaala wa Mafunzo ya Udereva kwa nadharia na vitendo ikiwemo mbinu
mbalimbali katika fani ya Udereva wa Magari ambapo jumla ya Wanafunzi
125 wamehitimu Mafunzo hayo miongoni mwao Wanaume ni 133 na wa kike ni
2.
Aidha
Kamishna Msaidizi wa Magereza, Nduguru alieleza changamoto mbalimbali
ambazo Chuo hicho kinakabiliana nazo ikiwemo upungufu wa magari ya
kujifunzia pamoja na uchakavu wa miundombinu ya majengo hali inayoathili
utoaji taaluma ya mafunzo hayo.
Chuo
cha Udereva na Ufundi cha Kingolwira, kilichopo Mkoani Morogoro
kinamilikiwa na Jeshi la Magereza ambacho hutoa Mafunzo ya Udereva kwa
Maofisa wa Jeshi la Magereza ambao huendesha magari ya Jeshi hilo na
katika Taasisi mbalimbali za Umma hapa nchini.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269