Naibu
Waziri wa Afya, .Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kigwangalla leo amewatembele wahanga wa ugonjwa wa kipindupindu
mkoani Iringa na kuwaeleza kuwa wasiwe na wasiwasi serikali ipo pamoja
nao na inafanya jitihada kuokoa maisha yao.
Pia
alieleza kwa sasa serkali inashughulikia uokoaji wa maisha na
inashughulikia suala la chakula na malazi na kwamba wananchi wanatakiwa
kunawa mikono vizuri ili kujiepusha na ugonjwa huo, ambao umesababishwa
na mafuriko ya mto Ruaha kutokana na maji kujaa na kuacha njia yake.
Kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini, Dkt. Ignas Mlowe alisema maji hayo yalisomba nyumba na kubomoa vyoo.
Kuafuatia
hali ya mafuriko Dkt. Kigwangalla aliamuru chopa iliyompeleka katika
tukio itumike kuwaokoa wakina mama wanne mmoja kati yao ni mjamzito na
watoto wanne mmoja wa mchanga wa wiki mmoja.
Alisema
ameridhishwa na huduma za uokoaji hivyo aliwataka wananchi kutoa
ushirikiano kwa waokoaji ili kutolifanya zoezi kuwa gumu.
Aliwasisitiza
wananchi hao kunywa maji kwa wingi kwani ni muhimu kwa maisha yao pia
alimwagiza Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini, Richard Kassela kuhakikisha
wananchi wanakuwa na vyoo na kufukia madimbwi ya machafu ili kujiepusha
na ugonjwa huo.
Nae Mkuu
wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alisema ugonjwa huo umeathiri watu 223
na kuua mtu mmoja pia wagonjwa waliolazwa kambini ni 40.
Na Magreth Kinabo, Maelezo
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269