Rais Bashar al-Assad wa Syria amesema mpango wa Saudi Arabia na
Uturuki kutaka kuingia kijeshi nchini Syria ulianza miaka miwili
iliyopita.
Rais wa Syria aliyasema hayo jana Jumatatu katika matangazo
yaliyopeperushwa kwenye runinga ya taifa ya nchi hiyo na kuongeza
kwamba, ni kutokana na azma hiyo ndiposa nchi mbili hizo zimekuwa
zikiunga mkono harakati za kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh nchini
Syria. Rais al-Assad amekariri kuwa, Syria ina hamu ya kuona mgogoro wa
nchi hiyo unamalizika haraka, lakini magenge ya kigaidi na waungaji
mkono wao hususan Saudi Arabia, wanakwamisha mazungumzo ya kuupatia
ufumbuzi mgogoro huo huku akisisitiza kuwa jukumu la kwanza la serikali
yake ni kulitokomeza kikamilifu kundi la kitakfiri la Daesh. Kauli ya
Rais al-Assad inajiri katika hali ambayo, Saudi Arabia na Uturuki
zimesema kuwa huenda karibuni hivi zikaanzisha mashambulizi ya nchi kavu
nchini Syria eti kwa lengo la kukabiliana na kundi la kigaidi na
kitakfiri la Daesh. Mevlut Cavusoglu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki
amesema Ankara na Riyadh zinajiandaa kwa operesheni ya ardhini nchini
Syria na kwamba ndege za kivita za Saudia tayari zimeanza kuingia katika
kambi ya Incirlik nchini Uturuki, ambayo kwa sasa inatumiwa na
Marekani, Ufaransa na Uingereza katika hujuma zao ndani ya Syria. Wakati
huo huo, mshauri wa masuala ya kisiasa wa Rais Bashar al Assad wa Syria
amesema kuwa, madai ya Marekani kwamba inapambana na ugaidi ni uongo
ulio wazi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269