Mgombea
urais wa chama cha upinzani cha FDC nchini Uganda Kizza Besigye
amekamatwa na kuzuiliwa kwa muda na maafisa wa polisi mjini Kampala.
Gari lake
lilikuwa likipitia barabara ya Jinja, mjini Kampala, msafara wake
ukisindikizwa na mamia ya wafuasi, pale polisi walipotumia mabomu ya
machozi kuwatawanya wafuasi hao na wakamkamata mwanasiasa huyo.
Alizuiliwa kwa muda katika kituo cha polisi cha Kira Road lakini akaachiliwa huru bila kufunguliwa mashtaka.
Polisi wanasema alikamatwa kwa sababu ya kutatiza uchukuzi mjini.
Bw Besigye alipangiwa kufanya mikutano ya kampeni katika mji huo mkuu.(VICTOR)
Wasifu wa Kizza Besigye Museveni: Nina imani nitashinda uchaguzi
Mkuu wa
Polisi Jenerali Uganda Kalekezi Kayihura amethibitisha kwamba polisi
walikabiliana na wafuasi wa upinzani lakini akakanusha habari kwamba
Besigye amekamatwa.
Jenerali
Kayihura Msemaji wa polisi Fred Enanga amesema Besigye alikaidi agizo
la polisi la kutoingia katikati mwa mji na ndio maana akakamatwa.
“Besigye
yuko huru kufanya kampeni mjini Kampala lakini sharti atii maagizo ya
Tume ya Uchaguzi na Polisi ambayo yanaharamisha siasa katikati mwa
jiji,” ameambia wanahabari.
Amesema
alizuiwa kwa muda kutumia barabara ya Nasser na kwamba polisi
walimzuilia wakihofia usalama wake baada ya kushindwa kudhibiti umati.
Hali ya
wasiwasi ilitanda katika maeneo ya Kampala huku polisi wakitumia mabomu
ya machozi kuwatawanya watu. Watu kadha walikamatwa.
Baada ya
kuachiliwa, kiongozi huyo wa upinzani aliruhusiwa kuendelea na kampeni
zake hadi chuo kikuu cha Makerere huku polisi wakiendelea kushika doria.
Bw
Besigye, alikuwa wakati mmoja daktari wa kibinafsi wa Bw Museveni,
amekamatwa na kuzuiliwa mara nyingi lakini Jumatatu ilikuwa mara ya
kwanza kukamatwa wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka huu.
Uchaguzi huo utafanyika Alhamisi.
Besigye amewania urais mara tatu dhidi ya Bw Museveni bila mafanikio.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269