Profesa Ndalichako
Na
JacquilineMrisho MAELEZO
Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Prof.Joyce Ndalichako
amesitisha mkataba wa ajira wa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo, George
Nyatega pamoja nakuwasimamisha kazi Wakurugenziwatatu.
Ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam alipokuwa akiongea na waandishi
wa habari ofisini kwake kuhusu matatizo ya kiutendaji na matumizi mabaya ya
fedhazaUmmayanayofanyikaBodiyaMikopo.
Prof.Joyce Ndalichako amesema kuwa Taasisi ya Bodi ya Mikopo imeonesha
utendaji usioridhisha kiasi kwamba kumekuwa na matatizo mengina
yanayojirudiarudia kwa wateja wao mara kwa mara.
“Mikopo kwa wanafunzi imekuwa ikichelewa kuwafikia bila sababu za msingi
kiasi kwamba imejengeka taswira kwa wanafunzi kwamba hadi walalamike wizara ni
ndipo matatizo yao yashughulikiwe hivyo, tatizo sio ukosefu wa fedha bali ni
uzembe wa watendaji katika kuwapatia wanafunzi mikopo yao kwa wakati.”AlisemaNdalichako.
Amewataja watumishi aliowasimamisha kazi kuwa ni Mkurugenzi wa Fedha na
Utawala Yusuph Kisare, Mkurugenzi wa Urejeshaj iMikopo Juma Chagonja pamoja na
Mkurugenzi wa Upangaji na Utoaji Mikopo Onesmo Laizer.
Aidha,amezitaja baadhi ya sababu zilizosababishwa kufukuzwa na
kusimamishwa kazi kwa watumishi hao zikiwemo za kufanya malipo yasiyo sahihi
kwa baadhi ya wanafunzi wanaosoma ndani na nje ya nchi pamoja udhaifu uliobaini
kakatika mifuko ya fedha.
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu inajukumu la kutoa mikopo kwaajili ya
wanafunzi wa elimu ya juu na kusimamia urejeshaji wa mikopo hiyo, kwa mwaka wa
masomo 2015/2016 jumla ya Shillingi Bilioni 459 imetolewa mikopo kwa wanafunzi
122,486 wanaosoma katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269