Mmoja wa Mashabiki wa Tamasha la Pasaka pamojana mashabiki
wengine waliohudhuria katika Tamasha la Pasaka lililofanyika mjini Geita
Mkoani Geita kwenye ukumbi wa Desire wakiimba kwa kuzinguka ukumbi huo
wakati mwimbaji Upendo Nkone alipokuwa akifanya vitu vyake jukwaani na
kuwafanya wavutiwe na tamasha hilo kiasi cha kushindwa kukaa kwenye viti
wakizunguka huku na kule huku baadhi wakiwa wabebeba viti juu juu,
Katika Tamasha hilo mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Geita
Manzie Mangachie akizungumza na mashabiki wa muziki wa injili
waliohudhuria katika tamasha hilo ameishukuru kampuni ya Msama Promotion
na Mkurugenzi wake Bw. Alex Msama kwa kuandaa tamasha hilo kwani hiyo
ni fursa pekee ya baadhi ya wananchi wa mkoa wa Geita kumrudia Mungu na
kutubu ili kuacha tabia mbaya inayoupaka matope mkoa huo kwa mauaji ya
walemavu wa ngozi Albino pamoja na Vikongwe
Waimbaji mbalimbali wameshiriki katika tamasha hilo ambao ni
Upendo Nkone, Bonny Mwaiteje, Joshua Mlelwa, Martha Baraka, Jesca BM,
Jennifer Mgendi, Mwimbaji kutoka Zambia Ephraim Sekereti, Waimbaji
kutoka Nchini Kenya Solomon Mukubwa , na Mtanzania Faustine Munishi
pamoja naye Christopher Muhangila.
Matamasha hayo yataendelea kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini
Mwanza na keshokutwa litafanyika tamasha lingine kama hilo mjini Kahama
mkoani Shinyanga.
Tamasha la Pasaka linaandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion
chini ya mkurugenzi wake Bw. Alex Msama kwa udhamini wa magazeti ya
Dira, Dira TV na Dira FM na linafanyika kila mwaka katika kipindi cha
sikukuu za Pasaka (PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-GEITA)
Mwimbaji Jesca BM akifanya vitu vyake jukwaani.
Mashabiki wake wakiitikia na kuimba kwa hisia wakati mmwibaji huo akiimba jukwaani.
Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw. Alex Msama akirekebisha sauti
katika mitambo wakati tamasha hilo likiendelea huku DJ akiangalia.
Mama akifurahia uimbaji na uponyaji kutoka kwa waimbaji katika tamasha hilo huku akiwa amemshikilia mtoto wake mchanga.
Maadhi ya mashabiki wa muziki wa injili wakifuatilia waimbaji kwa makini.
Mwimbaji Martha Baraka na kundi lake wakitumbuiza jukwaani huku baadhi yamashabiki wakipata picha kwa simu.
Mwimbaji Jennifer Mgendi naye akafanya mambo makubwa jukwaani kama anavyoonekana.
Mwimbaji Ephraim Sekereti akisalimiana na mdau mkubwa wa Msama
Promotion Bw. Silas huku akitaniana na Mkuu wa Wilaya ya Geita Manzie
Mangachie wa tatu kutoka kushoto waliosimama mara baada ya kumaliza
kuimba.
Mwimbaji Solomon Mukubwa kutoka nchini Kenya akiimba jukwaani huku mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Geita Manzie Mangachie akicheza pamoja na Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw. Alex Msama na mashabiki wengine.
Mwimbaji Solomon Mukubwa kutoka nchini Kenya akiimba kwa hisia mbele ya mashabiki wake walioonekana kuhamasika na nyimbo zake.
Mwimbaji Bonny Mwaiteje naye akafanya mambo makubwa jukwaani huku akipewa sapoti na mashabiki wake.
Mwimbaji Bonny Mwaiteje akiwa amewabeba wacheza shoo wake mara
baada ya kumaliza kuimba jukwaani hii ilikuwa ni staili ya aina yake.
mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Geita Manzie Mangachie
akitoa salamu zake za shukurani kwa kampuni ya Msama Promotion kwa
kuandaa tamasha la pasaka katika mkoa wa Geita wilaya ya Geita kwa ni
jambo jema kuwahubiria amani wananchi wa Geita ili wamrudie Mungu na
kuacha mauaji ya Albino na Vikongwe.
Waimbaji Solomon Mukubwa kulia , Bonny Mwaiteje kushoto
wakimpiga tafu Mwimbaji mwenzao Christopher Muhangila katikati wakati
alipokuwa akitumbuiza jukwaani
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269